30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yasimika bendera Mlima Kilimanjaro

*Wafanyakazi wahamasisha utalii wa ndani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
 
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wamefanikiwa kupanda na kusimika bendera ya taasisi hiyo kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
 
Benki hiyo pia imelitumia tukio hilo kama sehemu ya kuwahamasisha wafanyakazi wake na Watazania kwa ujumla kushiriki utalii wa ndani ili kusaidia kukua kwa shughuli hiyo yenye fursa lukuki kibiashra na tija kiuchumi.
 
NMB imeanza rasmi kushiriki kuutangaza utalii wa ndani hivi karibuni na kutangaza kushiriki kusaidia kuchangia kukua kwake Jumamosi iliyopita huko Moshi wakati wa kuwapokea wafanyakazi wake sita waliofanikiwa kupanda mlima huo.
 
Akizungumza kwenye hafka hiyo iliyofanyika kwenye lango la Mweka, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya NMB, Dismas Prosper, alisema timu ya watu sita iliyokwea mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika ilitumia siku saba kumaliza zoezi jilo.
 
Alisema kufanikiwa kwa timu hiyo kusimika bendera ya NMB kwenye Kilele cha Uhuru ni jambo kubwa kwa wafanyakazi hao na benki hiyo ambayo ndiyo kinara katika shughuli na huduna za kifedha nchini.
 
“Kwanza kabisa, dhamira ya safari hii ni kufanikiwa kuupanda Mlima Kilimanjaro na kusimika bendera ya Benki ya NMB kwenye kilele chake kama namna ya kipekee kwetu kusherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja,” Prosper alibainisha.
 
“Pia uongozi wa NMB unalitumia zoezi ili la kuupanda Mlima Kilimanjaro kuhamasisha utalii wa ndani na kuchangia maendeleo ya shughuli za kitalii nchini,” kiongozi huyo alisema.
 
Prosper alisema pia kuwa na tukio la kusherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja mita 5,895 juu ya usawa wa bahari kuna maana kubwa kwa namna benki hiyo inavyozingatia huduma bora kwa wateja na katika nafasi yake kama kiongozi wa kibenki sokoni.
 
Aidha, ni kitendo cha kutambua umuhimu wa biashara wa utalii na jukumu la msingi sekta hiyo katika uchumi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
 
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Iman Kikoti, alisema kitendo cha wafanyakazi wa NMB kupanda Mlima Kilimanjaro kinaimarisha nafasi ya benki hiyo kuendelea kuwa karibu na sekta ya utalii na mshirika wa kimkakati wa maendeleo ya taifa.
 
Pia alibainisha kuwa uamuzi wa NMB wa kuhamasisha utalii wa ndani ni kielekezo cha utayari wake kuchangia maendeleo na ustawi wa tasnia hiyo ili iweze kuchangia kikamilifu kuchochea kukua kwa uchumi nchini na ujenzi wa taifa.
 
Kikoti alipongeza NMB kwa hilo alisema utalii wa ndani ni hazina kubwa kwa taifa ambayo inahitaji ushirikiano wa wadau kuufanya kushamili na kuchangia kukua kwa sekta nzima ya utalii nchini.
 
“Kwa sasa mchango wa utalii bado ni mdogo kwa hiyo uamuzi wa NMB kusaidia kuuchangamsha ni jambo jema na la kimaendeleo linalopaswa kuungwa mkono na wadau wote wa sekta binafsi,” alibainisha.
 
Kiongozi wa safari hiyo iliyoanza tarehe Oktoba 8, kwenye Lango la Machame, Alfred Shayo ambae pia ni Afisa mkuu wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, alisema kamwe hawatajutia kushiriki kwenye zoezi hilo lilowafunza mambo mengi ya kimaisha na kikazi
 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles