24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yaikabidhi vifaa Bunge Sports tayari kwa Tamasha la Kivumbi na Jasho J’mosi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

BENKI ya NMB, leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu saba za Bunge Sports Club, zinazoundwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Tamasha la la NMB na Bunge lenye kauli mbiu ya Kivumbi na Jasho.

Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Abass Tarimba (Katikati) kwa ajili ya Tamasha la NMB na wabunge litalofanyika kesho katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kushoto ni Mwakamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club – Esther Matiko.

Michezo hiyo itafanyika baina ya waheshimiwa wabunge na wafanyakazi wa benki ya NMB ikiwa pia ni maandalizi ya Mbio za NMB Marathon 2021 zitakazo fanyika jijini Dar es Salaam tarehe 18 mwezi huu.

Tamasha la Kivumbi na Jasho, linatarajia kufanyika Jumamosi Septemba 4, kwenye viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema licha ya kutumika kujenga mahusiano mema baina ya taaisi hizo, tamasha hilo ni sehemu ya juhudi za benki ya NMB kuhakikisha jamii ya Kitanzania inapenda michezo, ambayo ni muhimu kwa afya na pia ni ajira.

Alisema wanajisikia furaha kupata nafasi adhimu ya kujumuika pamoja na watunga Sheria hao, ambao Wengi wao ni wateja wao, hivyo wanaushukuru uongozi wa Bunge na Kamati ya Utendaji ya Bunge Sports kwa kukubali kutenga muda wa kushiriki Tamasha hilo.

“Vifaa tunavyokabidhi leo ni pea 20 za tracksuit, seti moja ya jezi za netiboli, pisi 15 za basketball, mipira 6, pea 16 za jezi za soka, pea 10 za kikapu wanawake, jezi za kukimbilia pisi 200. Vyote hivi vina thamani ya Sh milioni 12,” alisema Mponzi mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Sports, Tarimba Abbas, ambaye ni Mbunge wa Kinondoni.

“Tutalianza Tamasha la Kivumbi na Jasho kwa mbio za taratibu ‘jogging’ asubuhi kuanzia viwanja vya Bunge hadi Chinangali Park,  kisha michezo mingine ikiwamo kuvuta kamba, kikapu, netiboli, wavu, kukimbiza kuku na mwisho mpira wa miguu na kukabidhi zawadi washindi,” aliongeza Mponzi, ambaye alisema watalitumia Tamasha hilo kujiandaa na mbio za NMB Marathon 2021, zitakazofanyika Dar es Salaam Septemba 18 mwaka huu.

Akitoa neno la shukrani, Tarimba aliipongeza NMB kwa dhamira ya dhati ya kuimarisha mahusiano baina ya taasisi hizo kiasi cha kuwaandalia tamasha hilo na kwamba Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesisitiza na kuonesha umuhimu na thamani ya Kivumbi na Jasho, lililokuwa lifanyike Juni mwaka huu, lakini likaahirishwa kutokana na msongo wa majukumu yao kibunge.

“Wabunge wakiwa hapa wanakuwa bize kiasi cha kuchoka kimwili na kiakili, kwa hiyo wanahitaji utimamu unaopatikana kupitia mazoezi yanayoenda kufanyika kupitia tamasha hili, ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku, ndio maana tumelipa heshima kubwa na kukubali uwepo wake.

“Taasisi nyingi na mashirika mengi yalituomba kushirikiana nasi kimichezo, lakini msongo wa majuku ukatulazimisha kukataa, lakini umuhimu wa NMB kwa jamii na Wabunge, ukatusukuma kukubaliana nalo, ingawa tukawapa masharti ya kutoleta ‘mamluki’ Kama walivyofanya wengine,” alisisitiza Tarimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles