24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wahimizwa kuelimisha watoto wa kike

Na Shomari Binda,Musoma

WAZAZI na walezi wamehimizwa kuhakikisha wanasimamia elimu na malezi bora kwa mtoto wa kike ili kutimiza ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Baraza Kuu la Wanawake (UWT) Taifa Mkoa wa Mara, Rhobi Samwel,katika kikao cha Baraza la Wanawake Manispaa ya Musoma kilichofanyika jana.

Amesema elimu ni muhimu na urithi mkubwa utakaomsaidia mtoto wa kike na baadae kuwa mama bora.

Rhobi amesema mtoto wa kike amekuwa na changamoto nyingi zikiwamo za kufanyiwa vitendo vya ukatili hivyo elimu ndio njia pekee ya kuwasaidia.

Amesema kila mzazi na mlezi analo jukumu la kuhakikisha ndoto za mtoto wa kike zinafanikiwa na moja ya njia ni kupata elimu.

“Ndugu zangu kina mama wajumbe wa Baraza la Wanawake Manispaa ya Musoma nawashukuru kwa kunialika kama mgeni rasmi lakini moja ya ujumbe wangu ni kusisitiza elimu kwa watoto wetu wa kike.

“Watoto wote wanastahili elimu lakini mtoto wa kike amekuwa na changamoto kwenye jamii zetu na wanapaswa kushikwa mkono,”amesema Rhobi.

Amesema yupo tayari kufadhiri elimu ya uandishi wa habari kwa watoto wawili wa kike na kuwaomba wajumbe hao kuwatafuta wenye vigezo ili kuwasaidia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Juiya ya Wanawake (UWT) Manispaa ya Musoma, Stella Mtani,amesema wanaendelea kuwasisitiza Wanawake na jamii kuendelea kuchanja chanjo ya Corona na salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles