30.2 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NMB CDF Trophy 2023 kulindima Septemba 2 Lugalo

Na Wainfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Shindano la Gofu la Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF Trophy’, linatarajia kutimua vumbi Septemba 2 -3, 2023 likishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka klabu za Tanzania na Malawi kwenye viwanja vya gofu Lugalo, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo amesema jana jijini Dar es Salaam kuwa lengo la shindano hilo ni kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Amesema kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo ni NMB ambao wamekuwa wakishirikiana nao kwa miaka nane sasa.

‘Huu ni mfululizo wa udhamini wa NMB na mwaka huu shindano litakuwa la kipekee kutokana na maboresho waliyofanya hasa katika zawadi na tunategemea mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Majeshi mwenyewe,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wateja Binafsi wa benki ya NMB, Aikansia Muro, katika udhamini huo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 30 kufanikisha shindano hilo kutokana na kutambua umuhimu wa mchezo wa gofu ambao umeanza kupata wafuasi wengi.

“Udhamini huu ni katika kuendeleza na kutambua umuhimu wa mchezo nchini na lengo la kusapoti michezo mbalimbali ni kuwafikia Watanzania wengi zaidi,” amesema Aikansia.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga amesema wataendelea kushirikiana na wafadhiri mbalimbali wanaojitokeza ili kufikia malengo wanayohitaji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles