24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Waogeleaji wafurahia mpango wa HPT

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digitall

Waongeleaji kutoka klabu mbalimbali nchini wamefurahia uwepo wa programu ya mazoezi inayoendeshwa na taasisi ya ‘High Performance Training(HPT)’ kutokana na kuendelea kuimarisha viwango vyao vya uogeleaji.

HPT ambao ni wadau wa mchezo huo, juzi waliandaa mashindano yaliyowakutanisha waogeleaji kutoka klabu za Tanzania Bara na Zanzibar baada ya kumaliza kambi ya mafunzo ya wiki sita ya kuwanoa wanamichezo hao.

Mashindano hayo ya msimu wa nne yalifanyika katika bwawa la shule ya Kimataifa ya Tanganyika, Masaki, Dar es Salaam.

Akizungumzia mashindano hayo, muiogeleaji wa Kimataifa wa Tanzania, Collins Saliboko, amesema hiki ndio kipindi chao cha kuogelea kwa kushiriki mashindano mengi katika kujiandaa kuelekea michezo ya Olimpiki 2024 itakayofanyika Paris, Ufaransa.

“Kwa sasa hivi msimu wa kwetu wakuogelea sisi wa Watanzania ndio umeanza, najiandaa ili nifanye vizuri katika mashindano yanayofuata. Tuna miezi kama tisa tu imebaki kufika Olimpiki 2024 Paris, nataka kuwa Mtanzania wa kwanza kufikia muda mzuri,” amesema Saliboko.

Naye Lina Goyayi, amesema HPT imewasaidia kupunguza muda wao na kuwajengea uwezo wa kuwa waogeleaji wazuri ambao baadaye wataweza kushindana katika mashindano makubwa.

Aidha Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro, ameweka bayana kufurahia uwepo wa mashindano hayo na kambi ya HPT kwani yanakusanya waogeleaji wengi, ikiwa ni mara ya nne kufanyika wameona matokeo yake kwa waogeleaji wa Tanzania kufanya vizuri Kimataifa.

“Kwa kawaida katika mpango huu waogeleaji wanatumia wiki sita wanafanya mazoezi asubuhi na jioni na baada ya hapo ndio yanafanyika haya mashindano, kwa kweli tumeona maendeleo ni mazuri na watoto wamekuwa wakipunguza muda wao vizuri,” amesema katibu huyo.

Amefafanua kuwa lengo la TSA ni kuona wachezaji wafanya mazoezi zaidi na kushiriki mashindano ya mara kwa mara ili kuwa na waongeleaji wengi wa kushindana Kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles