26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Nkana waitisha Simba

Na HUSSEIN OMAR-DARES SALAAM

KOCHA wa Nkana FC ya Zambia, Beston Chambesh, amewaonya wapinzani wao Simba watakaokutana katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwaambia kikosi chake kipo imara na wamepanga kufika mbali katika michuano hiyo.

Simba imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1 ikishinda mabao 4-1 nyumbani jijini Dar es Salaam na mabao 4-0 ugenini Jumanne iliyopita.

Kutokana na ushindi huo, Wekundu hao wa Msimbazi watawakabili Nkana kati ya Desemba 14 na 16 mjini Kitwe na mchezo wa marudiano utachezwa kati ya Desemba 21 na 23 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Chambesh aliliambia gazeti la Daily Mail la Zambia kuwa kikosi chake kipo imara na kina uwezo wa kufanya jambo lolote nje na ndani katika michuano hiyo mwaka huu.

“Nimeridhishwa na vijana wangu jinsi walivyocheza, nina uhakika mwaka huu tutafika mbali zaidi kwani tumejipanga kufanya vizuri katika kila mchezo tutakaocheza,” alinukuliwa Chambesh.

Chambesh alisema kuelekea katika mchezo huo, amejipanga kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha anautumia vyema uwanja wa nyumbani kupata ushindi mnono.

Hii ni mara ya tatu kwa Nkana kupangwa na Simba kwenye hatua mbalimbali za mashindano ya kimataifa ambapo kabla ya hapo walipangwa mwaka 1994 na 2002.

Katika Kombe la Washindi mwaka 1994, Simba ambao walikuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ilitolewa na Nkana kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 kwenye robo Fainali ya Kombe la Washindi Afrika.

Nkana ilianza kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mechi ya kwanza Zambia na walipokuja nchini mchezo wa marudiano Simba ilishinda mabao 2-0.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles