24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NJIA ZA KUKUMBUKA KILA KITU UNACHOJIFUNZA – 2

Pombe huathiri uwezo wa mtu wa kumbukumbu.
Pombe huathiri uwezo wa mtu wa kumbukumbu.

Na JOACHIM MABULA,

TULIANZA makala haya kwa kuangalia njia ambazo mtu anaweza kutumia kuboresha kumbukumbu  zake pindi anapojifunza. Tuliona njia za kukumbuka mambo mbalimbali unayojifunza kama vile kujilazimishe kukumbuka, kutochukulia mambo kiwepesi, kuunganisha jambo jipya na mambo ya kale.

Leo tutaangalia mambo mengine yanayoweza kukusaidia.

Tafakari

Pendezwa na kile unachofundishwa na ikiwezekana andika kile unachojifunza kwa maneno yako. Kuandika mambo makuu husaidia msikilizaji kukaza fikra na pia kurudia habari hiyo baadaye. Ukiwa na mambo makuu kwenye fikra zako hukusaidia kutafakari.

“Wakati watu wanapopata nafasi ya kutafakari, huongeza uzoefu katika ufanisi binafsi,” Profesa Francesca Gino wa Shule ya Biashara ya Harvard anasema. “Wao huhisi kujiamini zaidi kufikia malengo yao. Matokeo yake wao huweka juhudi zaidi katika kile wanachotakiwa kufanya na kile wanachojifunza.

Mambo mengine yanayoweza kukusaidia

Kujifunza kitu kipya mfano ufundi fulani, lugha mpya au kucheza ala ya muziki huchochea kumbukumbu. Jifunze mbinu za kutumia herufi za kwanza za neno au za fungu la maneno kutokeza neno jipya.

Kunywa maji ya kutosha. Upungufu wa maji mwilini unaweza kumfanya mtu achanganyikiwe. Lala vya kutosha. Mtu anapolala ubongo wake huhifadhi habari katika kumbukumbu. Epuka mambo yanayofadhaisha unapojifunza kwani mfadhaiko huchochea homoni inayoitwa cortisol inayoweza kuzuia neva kupitisha habari.

Epuka kulewa na kuvuta sigara kwani pombe huathiri uwezo wa mtu wa kukumbuka mambo, na uraibu wa kileo unaweza kupunguza vitamini B ambayo ni muhimu ili mtu awe na kumbukumbu bora. Kuvuta sigara hupunguza oksijeni kwenye ubongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles