26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Nitatangaza kugombea urais muda ukifika – Ngeleja

William Ngeleja
Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja

NA PETER FABIAN

MBUNGE wa Jimbo la Sengerema , William Ngeleja (CCM), amesema anangoja muda uwadie ili naye atangaze nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu mwakani kwa vile sasa kanuni za chama hicho haziruhusu.

Alisema kwa nguvu za Mungu anaamini atadumu mpaka kipindi hicho (mwakani) kwa vile anao uwezo na nia hivyo atatangaza kugombea nafasi ya hiyo ya urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ngeleja alisema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji na Kata ya Kishinda wilayani Sengerema.

Aliyasema hayo baada ya Katibu wa CCM wa Kata hiyo, Anthony Ndumila kumwambia kuwa wananchi wa Kishinda wanamuombea awe rais wa awamu ya tano.

Awali Ndumila alimtaka atamke iwapo atagombea ili wagombea wengine waliokwisha kutangaza ama kuonyesha nia watambue mbunge wao Ngeleja naye yumo katika kinyang’anyiro hicho.

Ngeleja ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) katika wilaya hiyo, alisema ana haki ya kuwania nafasi ya urais ndani ya chama chake na wakati wa kufanya hivyo ukifika hafichi.

“Wananchi wengi wamekuwa wakinieleza niwanie tena ubunge wa jimbo hili ili niendelee kuwa mwakilishi wao lakini pia baadhi wanaomba niwanie nafasi ambayo bado sijatangaza rasmi kwani wakati ukifika naweza nikafikilia kukubaliana na mawazo yao kama nilivyokubaliana na wengine na kugombea ubunge wa jimbo hili na kushinda.

“Nafahamu wengi wenu leo mlitamani kusikia hayo yanayoandikwa na vyombo vya habari nchini yatimie lakini kuweni na subira kwani kila mwana CCM anayo haki ya katiba ya kuwania nafasi yoyote,” alisema.

Ngeleja ni miongoni mwa makada wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi ya urais ndani ya chama hicho ambao hata hivyo walizuiliwa kwa mwaka mmoja kufanya kampeni za chini chini za kuwania kuungwa mkono kugombea nafasi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles