GLORY MLAY
MSANII wa miondoko ya Hip Hop Bongo, Nikki Mbishi, amesema anatamani kuona wakongwe wa muziki huo Profesa Jay na Sugu (Jongwe), wakianzisha kampuni za kusaidia tasnia na siyo kutoa nyimbo za kushindana na wasanii wapya.
Akizungumzia hilo, Nikki Mbishi alisema wasanii hao ambao pia ni wabunge wa majimbo tofauti wana nafasi na uwezo mkubwa wa kuwekeza kwenye tasnia.
“Sitarajii kuona wasanii hawa wanatoa ngoma na wanashindana kwenye chati na kina Country Boy au wasanii wengine, tunatamani kuwaona kama ma C.E.O,” alisema.
Nick Mbishi aliongeza kuwa huu ni muda wa Profesa Jay na Jongwe kushirikiana na wasanii kwa kuwa wana nafasi hoyo sasa.