28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

NIDHAMU NI MUHIMU NGAO YA JAMII

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MASHABIKI wa soka hapa nchini kwa sasa wanasubiri siku ya pambano kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga, ifike ili kufahamu mbabe ni nani.

Mchezo huo wenye upinzani mkali, umepangwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ikiwa zimebaki siku mbili kufanyika kwa mchezo huo, suala zima la nidhamu ni kitu pekee kinachoweza kuimarisha amani katika mchezo huo kutoka pande zote.

Tunapozungumzia nidhamu si kwa wachezaji pekee, bali pia jambo hili linawagusa mashabiki ambao hakika watajitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo.

Inafahamika wazi Uwanja wa Taifa, una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000, hivyo ni jambo la busara kila atakayejitokeza kuhakikisha anazingatia sheria husika.

Matukio ya aibu yamekuwa yakitokea pindi Simba na Yanga zinapokutana, huku mengine yakipelekea timu hizo kongwe hapa nchini kuzuiwa kutumia uwanja huo kwa muda.

Matarajio ya wengi ni kuingia uwanjani kuangalia kandanda safi itakayotolewa na wachezaji mbalimbali walioweza kusajiliwa ndani ya timu hizo, lakini linapofika suala la vurugu ni dhahiri inaonyesha wazi jinsi gani nidhamu imekosa nafasi.

Matamanio ya wengi ni kumfahamu mshindi aliyepatikana kwa haki bila ubabaishaji kutoka upande wowote, hivyo ni vyema waamuzi wakawa makini.

Waamuzi wamekuwa wakibeba furaha na uvumilivu wa mashabiki wa timu hizi mbili pindi zinapokutana, ikiwa yatafanyika makosa ya wazi yanayoashiria upendeleo lazima vurugu zitatokea.

Hivyo, ili kuepusha yote hayo ni vema kila mmoja atayekuwa ndani ya uwanja huo siku ya mchezo, kuzingatia nidhamu kwani inapokosekana hata heshima huondoka pia.

Mchezo huo ambao utafungua rasmi msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18, unatarajiwa kuonyesha taswira nzuri na mustakabali mzima wa soka la  nchi  yetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles