32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

NICOL YACHUNGUZA UPOTEVU WA BILIONI 10/-

NA TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


 

kaundaKAMPUNI ya Uwekezaji ya Wazawa (NICOL) imeanza uchunguzi wa hasara ya Sh bilioni 10 iliyopata baada ya kufanya uwekezaji mbaya katika kampuni mbili tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NICOL, Gideon Kaunda alisema uchunguzi huo utafanyika kwa   wiki mbili.

Alisema  baadaye  ripoti itakabidhiwa na wahusika watakaobainika  watawafungulia kesi mahakamani.

Alisema hadi kufikia Desemba 31, 2009, kampuni hiyo ilipata hasara kutokana na kuwekeza kwenye  kampuni ambazo baadaye zilifilisiwa na benki ambazo zilikuwa zikizidai.

“NICOL iliwekeza Dola za Marekani milioni mbili (Sh  bilioni 4) katika kiwanda cha kutengeneza dawa kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro ambacho kilikopa benki ya Barclays.  Baada ya kushindwa kulipa deni kilitaifishwa  na kusababisha fedha hizi kupotea,” alisema Kaunda.

Alisema  NICOL iliwekeza Sh bilioni 3 katika kiwanda cha samaki   Mwanza na baadaye kukiongezea kiasi kama hicho kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB).

“Baada ya uwekezaji wa mwaka mmoja kilishindwa kulipa deni na kujikuta kinafilisiwa na benki.

“Mbali na kuwapo matumizi mabaya ya fedha, kodi za Serikali na michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi za jamii ilikuwa haipelekwi jambo ambalo liliongeza madeni,” alisema Kaunda.

Alisema katika uchunguzi huo, wataangalia upya mikataba ya kampuni za nje zinazonunua nyama iliyoingiwa na TMC kutokana na kuwa na upungufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles