ALIYEKUWA mpenzi wa marehemu Kristina Brown, Nick Gordon, amesema hawezi kuishi bila mpenzi wake huyo.
Gordon aliandika katika ukurasa wake katika mtandao wa Twitter kwamba ataendelea kumkumbuka mpenzi wake na mama mkwe wake, Whitney Houston, aliyefariki mwaka 2012.
“Nitaendelea kumkumbuka Kristina na mama yake kwa kuwa nilikuwa nawapenda sana, nilikuwa siwezi kufanya lolote bila Kristina.
“Kila siku wakati wa kulala mawazo yangu mengi ni juu ya Kristina, nitapotea katika maisha haya bila yeye, nataka arudi duniani,” alisema Gordon.