28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

NIC, GRR waingia makubaliano ya udhamini mbio za Goba Hills

Na Imani Nathaniel, Dar es Salaam

Kampuni ya Bima ya NIC imeingia udhamini wa miaka mitatu katika mbio za Goba Hills (Goba Hills Marathon), Udhamini huo unaogharimu fedha taslimu Sh milioni 25 kufikia kikomo mwaka 2023.

Udhamini huo umeingiwa leo Januari 7, jijini Dar es Salaam ambapo kampuni NIC itakuwa ndiyo mdhamini mkuu wa mbio hizo ambazo kwa mwaka huu zinabeba kauli mbiu ya ‘Kimbia, Okoa Maisha ya Mama na Mtoto’.

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dk. Elirehema Doriye amesema kampuni yao inajivunia kuwa mdhamini Mkuu wa mbio hizo.

“Tnayofuraha kubwa kushirikiana na waandaaji Goba Road Runners kwa kudhamini mbio za Goba Hills Marathon kwa mwaka huu baada ya mbio hizi kufanyika mwaka jana kwa mafanikio makubwa.

“Nia yetu kama kampuni ni kuona maendeleo yenye tija kwenye michezo hapa nchini, ni matumaini yetu kuwa kwa kupitia mbio hizi za NIC Goba Hill Runners tutaweza kufanikisha hilo,” amesema Dk. Doriye.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Goba Hills Marathon, Benson Luoga amesema kuwa mbio hizo zitakuwa za kilomita 42.2 (Full Marathon), 21.1 10 na 5.

“Lengo Kuu la Goba Hills Marathon ni kuboresha Afya ya Mama na Mtoto kwa kuboresha Mazingira ya Hospitali haswa Wodi za Kujifungulia akina Mama.

Usajili kwa ajili ya kushiriki mbio hizi ni Sh 30,000 kwa kila mmoja na tayari umeshafunguliwa na washiriki wameanza kujisajili kupitia tovuti ya Club ya GRR ambayo ji www.grr.co.tz,”amesema Luoga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles