Na Ronald Kabyemera, Marekani
WIKI hii, vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimetawaliwa na habari kuhusu usajili unaofanywa na vilabu vikubwa vya Simba na Yanga.
Wakati vilabu hivyo vikiendelea kufanya usajili, Kombe la Kagame linaendelea jijini Dar es Salaam pamoja na Kombe la Dunia kule Russia lakini magazeti yetu bado yametaliwa na habari za usajili.
Hata hivyo, pamoja na yanayoendelea, inaonekana kuwa vilabu hivi viwili vina ugonjwa unaotakiwa kutibiwa. Ugonjwa huo ni ule wa kudhani kwamba vyenyewe haviwezi kujiendeleza isipokuwa tu kwa msaada wa matajiri fulani fulani.
Niseme wazi kwamba kumilikiwa au kufadhiliwa na matajiri ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa michezo. Tofauti kubwa iliyopo kati ya Tanzania na kwingineko ambako michezo imeendelea ni kwamba wenzetu, matajiri wanakimbilia kudhamini, hapa kwetu timu zinabembeleza matajiri.
Roman Abramovich kwa sasa ana mgogoro na mamlaka za Uingereza na tayari mmoja wa matajiri wa huko ametaka auziwe Chelsea. Kinachotakiwa ni klabu na tajiri anaweza kuja na kuondoka.
Hali ni tofauti hapa kwetu. Ukiuliza chanzo cha matatizo ya kifedha yanayoikumba Yanga hivi sasa utaambiwa ni mfanyabiashara Yusuf Manji. Wapo wana Yanga wanaoamini kwamba klabu yao haiwezi kufanya chochote pasipo Manji. Ni kana kwamba Yanga haikuwahi kuwepo kabla yake.
KWA HABARI ZAIDI PATA NAKALA YAKO LA GAZETI LA MTANZANIA