29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

NHIF yamuenzi Nyerere kwa kutoa huduma bure

Na GUSTAPHU HAULE, PWANI

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Pwani umetumia siku ya maadhimisho ya miaka 21 ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kutoa huduma ya matibabu bure kwa Wananchi .

Maadhimisho hayo yaliyofanyika jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Majengo vilivyopo wilayani Bagamoyo, yalihusisha viongozi mbalimbali wa kichama na kiserikali.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja wa NHIF mkoa wa Pwani, Ellentruda Mbogoro, alisema kuwa wameamua kutumia fursa hiyo ili kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo.

Mbogoro alisema kuwa NHIF inatambua umuhimu wa afya kwa jamii na wao wamepewa dhamana ya kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za bima ya afya kwa karibu .

Alisema kuwa, miongoni mwa mambo ambayo Baba wa Taifa alikuwa akishughulikia ni pamoja na kuondoa  maradhi katika jamii na ndio maana Nhif imetumia fursa hiyo kikamilifu ili kuhakikisha jamii inapata uelewa zaidi.

Aidha, Mbogoro alisema kuwa pamoja na kutoa huduma ya matibabu bure lakini pia katika maadhimisho hayo walikuwa wakitoa elimu ya namna ya kujiunga na virufushi vya bima ya afya.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia NHIF imeweka mipango thabiti ya kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na matatibu kupitia bima ya afya ndio maana imekuja na mipango mbalimbali.

Mbogoro, alitaja miongoni mwa mipango hiyo kuwa ni Machinga afya, Bodaboda afya, Ushirika afya, Umoja  afya na Madereva afya na kusema makundi hayo yamezingatia hali halisi ya kipato cha kila mwananchi.

Hatahivyo,Mbogoro aliwataka wananchi na jamii kiujumla waliokuwepo katika makundi hayo kutumia fursa hiyo kikamilifu katika kuhakikisha wanakata bima zitakazowasaidia kulinda afya zao pale wanapopata maradhi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni, alisema kuwa ni Nhif wamekuwa mfano wa kuigwa na kwamba lazima wananchi waunge mkono juhudi hizo kwa faida ya afya zao.

Mgeni, alisema kuwa hakuna mafanikio bila kuwa na afya njema na kwamba njia pekee ni mtu kumiliki kadi ya matibabu ambayo itaweza kumsaidia pale anapougua.

Hatahivyo, Mgeni aliwataka wananchi hao kupima afya zao mara kwa mara ili kusudi wanapotambua kuwa na ugonjwa waweze kutibiwa kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles