31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaalamu aeleza maumivu yanavyoweza kumuimarisha mtu

Na SARAPHINA SENARA(UoI)-DAR ES SALAAM

MTAALAMU wa saikolojia kutoka chuo kikuu cha Iringa, Baraka Mushobozi  ameeleza faida za maumivu, akisema ni pamoja na kumuimarisha mtu kifikra na kumpatia wazo jipya ni namna gani anaweza kukabialiana na wakati anaopitia.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu, Mushobozi aliesema  maumivu yanayotokana na hisia mbalimbali kwa binadamu ambazo mtu amejitengenezea au wakati mwingine zinaweza kutokana na vitu  kama vile,vifo,kutendwa katika mahusiano pamoja na hisia nyingine zinazoleta maumivu.

Mushobozi alisema maumivu hayo hayawezi kuwa ya muda mrefu ama mfupi na yanaweza kuwa na nguvu sana ama yasiwe na nguvu sana na wakati mwingine yanaweza kujitokeza kupitia mfumo wako wa mwili.

“Faida mojawapo inayotokana na maumivu ni kumhimiza mtu kutafuta msaada kwakua inamfanya mtu apate msaada juu ya mfumo wa mwili  wake na  kutengeneza nafasi ya  kumshauri mtu kufanyia kazi katika jambo analoliona haliko sawa katika wakati anaopitia,”alisema Mushobozi. 

“Kumpa mtu nafasi ya kutafakari na faida yake ni kumfanya mtu azidi kukua katika lile eneo na kuwa imara kwa kumuimarisha mtu kumpatia wazo jipya kwa kufanya jambo kubwa zaidi ama kufanya kitu bora zaidi,” aliongezea.

Alisema maumivu yanaweza kumsaidia mtu kuwa na shauku ya kutafuta furaha na wakati mwingine hutumika kama sehemu ya kupeleka tarifa  sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumfanya mtu kupata wazo jipya hususani katika maaumizi fulani.

“Jambo lingine ambalo ni faida ya maumivu ni kukueleza sehemu isiyokuwa sawasawa au juu ya mfumoambao haquko sawasawa ili kufanyia ufumbuzi juu ya jambo hilo ili iwe rahisi kulifanyia kazi.

“Maumivu yana faida ya kumfanya mtu kuweza kuwa bora zaidi ya vile alivyokuwa mwanzo kutokana na kutafuta ufumbuzi aqmbao utaleta wazo jipya kwa mtu huyo na kumfanya aweze kuzidi kuimarika na kuboreka zaidi kutokana na wakati alioweza kupitia,” alisema. 

Maumivu yanapozidi yanaweza kutengeneza usugu katika jambo fulani ambalo lisipofanyiwa kazi linaweza kuleta madhara akwa mtu bhuyo kwasababu tu alishindwa kulifanyia kazi.

Alisema faida za maumivu ni nyingi sana inategemea tu na namna mtu anvyochukulia uzito juu ya jambo fulani na kuamua kuendelea na ukurasa mwingine usiokua na kasoro kwenye maisha yake.

“Watu wengi wanafikiri zaidi kuhusu hasara na kusahau kama kuna faida zake mdio maana ni vyema kuwashauri wasijione hawana thamani kwasababu tu hawawezi kustahimili hayo,” alisema Mushobozi.

“Ila kama mtu anaona hawezi kustahimili naunivu aliyokua nayo basi anaweza kuonana na wataalamu hasa wa masuala ya saikolojia ili aweze kupata msaada ni jinsi gani anaweza kunufaika na maumivu aliyonayo na namna anaweza kuimarika zaidi,” aliongezea.

Mushobozi aliwataka watu kuchukulia fursa changamoto wanazokutana nazo ili iweze kuwasaidia badala ya kubaki na maumivu yanayoweza kuwatesa maishani na kushindwa kuendelea katika maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles