28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ngw’anakilala kuzikwa leo

NA CHARLES MSETI, MWANZA

Nkwabi Ngw'anakilala
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Nkwabi Ngw’anakilala.

ALIYEKUWA Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Nkwabi Ngw`anakilala, anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake jijini Dar Salaam baada ya mwili wake kuagwa jana mkoani Mwanza.

Marehemu Nkwabi alifariki Juni 25, mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo.

Wakati wa uhai wake mbali na kuwa Mhadhiri wa SAUT pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa inatambulika kama TBC Taifa.

Mbali na hili pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) akiwa mratibu usambazaji wa habari na picha kuanzia mwaka 1994-1997.

Awali akisoma wasifu wa marehemu Mkuu wa Idara ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa SAUT, Imane Duwe, alisema marehemu alikuwa muadilifu katika utendaji wake wa kazi na kwamba alisimamia kuleta mabadiliko ya tasnia ya habari nchini.

“Tumepoteza mtu muhimu katika fani ya uandishi wa habari Tanzania na nje ya nchi, katika kipindi hiki kigumu tutamkumbuka kwa mambo makubwa aliyowahi kuyafanya katika taaluma ya uandishi,” alisema Duwe.

Mwili wa Ngw’anakilala unatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles