24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Homa ya dengue yaendelea kutesa Dar

Dar es Salaam
Eneo la katikati ya Jiji la Dar es Salaam

GRACE SHITUNDU NA MWAJUMA MALILO (DSJ)

WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kuendelea kuchukua hadhari na mbu aina ya Aides anayeeneza homa ya dengue kwa kuwa ugonjwa huo bado upo.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Daktari Kiongozi wa Idara ya Wagonjwa wa Nje wa Hospitali ya Mwananyamala, Mrisho Lupinda, alisema jamii inatakiwa kuendelea kuchukua hadhari ya ugonjwa huo kwa kuwa hauna chanjo wala tiba.

“Ugonjwa bado upo ingawa kwa sasa tunapokea wagonjwa wachache ambao ni kati ya mmoja mpaka watano kwa wiki moja, tofauti na kipindi kile cha mlipuko tulikuwa tunapokea wagonjwa zaidi ya saba kwa siku.

“Lakini kwa sasa inaonekana mbu hawa wanaoambukiza wamepungua kwani kwa siku tunaweza kupokea mgojwa mmoja au wawili na siku nyingine inapita pasipo kuwa na mgonjwa aliyeonekana kuwa na maambukizi ya dengue” alisema Dk. Lupinda.

Alisema pamoja na kupokea wagonjwa wachache watu wanaweza kupata maambukizi endapo jamii haitamdhibiti mbu huyo na homa ya dengue imekuwepo kwa zaidi ya miaka 300 lakini kwa Tanzania imeonekana kuwa tishio kuanzia Januari mwaka huu.

Homa ya dengue iliibuka mwezi Januari mwaka huu na kuonekana kuwa tishio miezi ya Aprili na Mei ambapo baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walifariki dunia huku wengine wakipata maambukizi na kulazwa katika hospitali mbalimbali za Wilaya na Taifa.

Mlipuko wa ugonjwa wa homa ya dengue ulilikumba Jiji la Dar es Salaam ambapo kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu zaidi ya wagonjwa 400 walithibitika kupata maambukizi ya ugonjwa huo huku wengine wakipoteza maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles