24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ngumi wahitaji mashindano ya majaribio ya kimataifa

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Kocha wa timu ya Taifa ya ngumi za Ridhaa, Hassan Mzonge, amesema wanahitaji mashindano mawili ya kimataifa ya majaribio ili kukiimarisha kikosi kiwe cha ushindani kwenye mashindano yajayo.

Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kusaka tiketi ya kufuzu michezo ya Olimpiki ambayo imepangwa kuanza Julia mwaka huu Tokyo nchini Japan.

Akizungumza na www.mtanzaniadigitl.co.tz Mzonge, amesema mashindano hayo yatasaidia kubaini kasoro na kuzifanyia kazi ili kukiweka tayari kikosi kimashindano.

Amesema kuwa tayari timu imeshiriki mashindano ya majaribio yaliyoshirikisha mabondia kutokaZimbabwe ambayo yalimalizika Jumanne ya wiki hii yamewaza kusaidia kutambua kasoro sasa zinakwenda kufanyika maboresho .

“Tunashukuru Mungu tumeshacheza shindano moja la majaribio ambalo kumekuwa na ushindani,lakini tukipata mashindano mawili kama hayo naamini timu utakuwa imeiva na tutakuwa tayari kupambana tupate nafasi kushiriki michezo ya Olimpiki,” amesema Mzonge.

Naye Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Mutta Rwakatare, ameiomba serikali kuangalia mchezo huo kwa jicho la tatu katika kuisaidia kuendesha mashindano mbalimbali.

Ameongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto ikiwamo uhaba wa vifaa vya michezo, fedha za kutekeleza shughuli za Shirikisho na ukosefu wa ufadhili.

Kwa upande wa mwakilishi wa Katibu MKuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Milinde Mahona, amesema amezipokea na atawasilisha Serikalini waweze kuona namna watakavyeweza kusaidia ili kuendeleza mchezo huo.

Amewata kuzigeuza changamoto hizo kuwa fursa ,hivyo wajipanga vizuri kimaandalizi ili waweze kufanya vizuri na kupata nafasi ya kufuzu michezo ya Olimpiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles