19.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ngoma, Tambwe mambo safi Yanga

Amissi Tambwe
Amissi Tambwe

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amissi Tambwe, amemaliza bifu na Donald Ngoma na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha timu hiyo kupata pointi tatu katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.

Nyota hao tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Yanga walipigana wakati timu ikiwa kambini nchini Uturiki na kuwekeana bifu, hali iliyomfanya kocha Hans van der Pluijm kuingilia kati ili kusuluhisha ugomvi wao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Tambwe ambaye aliumizwa vibaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu, alisema amemsamehe Ngoma na sasa anaungana naye ili kusaidia ushindi dhidi ya Medeama watakaovaana Juni 15, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Ugomvi wetu umekwisha sasa sina tatizo na Ngoma kwa sababu ni mchezaji mwenzangu ambaye tutashirikiana kwa pamoja kusaka ushindi katika mchezo dhidi ya Medeama ili kujiwekea mazingira mazuri zaidi.

“Mashabiki waondoe wasiwasi maana nafikiri jambo hili liliwaumiza sana na walikuwa wanasubiri kwa hamu kusikia tumefikia mwafaka, kwa sasa tutacheza kwa ushirikiano wa hali ya juu ili tufikie malengo yetu,” alisema Tambwe.

Ugomvi wa mastraika hao ulipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Yanga, kutokana na kutokea kipindi ambacho timu inakabiliwa na mechi ngumu za kimataifa na ushirikiano wao uwanjani ni muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles