Izzo Bizness: Nakuja na video ya Dangerous Boys

Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’
Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’
Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’

NA THERESIA GASPER

KUNDI la ‘The Amazing’ linaloundwa na msanii, Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’ na mwanadada Abela Kibira ‘Bella Music’, wanatarajia kuachia video na wimbo wao wa kwanza unaokwenda kwa jina la ‘Dangerous Boys’ hivi karibuni.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Izzo Bizness, alisema wameamua kuunda kundi hilo ili kuleta ladha tofauti katika muziki huu wa Bongo Fleva.

“Video hii imefanyika katika Studio ya Uprise Music chini ya Prodyuza Dupy huku video ikifanywa na Nick Dizzo wa Focus Films,” alisema.

Msanii huyo anayetamba na video ya ‘Shemu Lake’, aliwataka mashabiki wakae mkao wa kula kwani atawaletea kazi nzuri zaidi na zenye ubora mkubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here