Ngassa gumzo Etoile

0
1375

ngassaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA wa timu ya Etoile Du Sahel, Benzarti Faouzi amempigia saluti mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa kuwa ni mchezaji mwenye kasi na uwezo mkubwa.

Ngassa alionyesha kiwango kikubwa wakati timu yake ikivaana na Watunisia hao kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ulioisha kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya mchezo huo kocha huyo alisema, Ngassa ameweza kuendana na kasi waliyokuwa nayo wachezaji wake na ndiye mchezaji aliyewasumbua kidogo akishirikiana na Niyonzima na Msuva.

“Uwezo wao hautusumbui sana kwani na mimi wachezaji wangu ni wenye nguvu na wana uwezo mkubwa uwanjani na wanajua nini wanafanya licha ya kutofikia kiwango cha mabao tulichojiwekea,” alisema.

Akizungumzia mchezo kwa ujumla alisema, ulikuwa ni mzuri lakini mgumu sana kwani licha ya kucheza na timu nzuri lakini uwanja ulikuwa ukiwasumbua wachezaji wake kutokana na utelezi, hivyo wakati mwingine wanashindwa kufika mbali na mpira.

Alisema, sare hiyo sio mbaya zaidi na wanajipanga kuutumia vema uwanja wao wa nyumbani na kuongeza umakini zaidi kwani wanahitaji kusonga mbele zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here