26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ney wa Mitego: Mliooana heshimuni ndoa zenu

Ney wa Mitego
Ney wa Mitego

NA MWANDISHI WETU,

MKALI wa rap, Emanuel Eribariki ‘Ney wa Mitego’, amewataka wasanii waliooa na kuolewa kabla ya kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuendelea na wenzi wao hata mfungo huo utakapoisha.

Ney aliliambia MTANZANIA kwamba, wapo baadhi yao huolewa kila baada ya kuanza kwa mfungo huo jambo ambalo wanakuwa wakijidanganya wenyewe.

“Kama wameamua kuoa na kuolewa iwe kweli hata baada ya mfungo na si kuolewa ama kuoa baada ya mfungo wanaachana hilo litakuwa ni upuuzi na kujidanganya mwenyewe kwa kuwa imani ni kwamba anayeoa ama kuolewa amekubali hakulazimishwa hivyo inabidi atumikie ndoa yake kwa sheria za dini na si kuzikiuka.

“Nasema hivi kwa kuwa wapo baadhi yao waliolewa kipindi hiki ni kama tabia yao kwani mwaka jana kuelekea mfungo huu waliolewa na leo wameolewa tena, kwanini wanaendeleza tabia hizi badala ya kujitathmini kwanza kabla ya kukimbilia kuoa ama kuolewa,” alisema Ney wa Mitego.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles