NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Emanueli Elibariki ‘Ney wa Mitego’, amewataka wasanii wenzake kuwa na upendo na kutoa msaada kwa jamii.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ney alisema kuwa yeye ni kioo cha jamii na katika matatizo ya kibinadamu anakuwa kama mtu wa kawaida kwa kusaidia.
“Unajua sisi ni binadamu na kama umefanikiwa kwa kiasi fulani basi na wewe unatakiwa kutoa msaada kidogo ulichokua nacho, hivyo nawaasa wasanii wenzangu kujitolea,” alisema.
Msanii huyo amefanikiwa kufanya vizuri nchini kupitia nyimbo zake kama Akadumba, Nakula ujana na nyinginezo.