26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

NEMC yatakiwa kudhibiti usafirishwaji chuma chakavu

MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutumia ofisi zake za kanda kudhibiti usafirishwaji wa chuma chakavu maeneo yote ye mipaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam kujionea namna zoezi la usafirishaji wa chuma chakavu inavyoendeshwa, Waziri Simbachawene hakuridhishwa na utaratibu unaotumika sasa kusafirisha chuma chakavu kwani unachangia upotevu wa mapato ya serikali.

“Biashara hii inafaida kubwa kwa wafanyabiashara na utaratibu unaotumika sasa kusafirisha chuma chakavu hauisaidii serikali kupata mapato kupitia kodi kwa kuwa hakuna utaratibu wa kutoa risiti,” alisema Waziri Simbachawene.

Waziri alisema kuwa katika kipindi hiki ambapo azma ya serikali ni kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, chuma chakavu ni moja ya malighafi muhimu zaidi kwa viwanda vya hapa nchini.

“Chuma chakavu ambavyo inaruhusiwa kusafirishwa nje ya nchini ‘cast iron’ lakini vyuma vingine vyote lazima vibaki hapa nchini kwani hata viwanda vya ndani vimekuwa na uhitaji mkubwa wa chuma hivyo,” alisema na kuongeza kuwa NEMC lazima wajipange kudhibiti usafirishaji wa chuma chakavu.

Simbachawene mbali na kuiagiza NEMC kutumia ofisi zake za kanda, aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kusaidia kudhibiti usafirishaji wa chuma chakavu katika maeneo yao, na hasa mipakani ili kuzuia upotevu wa mapato ya serikali.

Aidha, Waziri ametoa muda kwa mamlaka husika kutoa maelezo ya kina kuhusu makontena 18 ya chuma chakavu yaliyosafirishwa nje ya nchi licha ya kuwepo kwa zuio la kusafirishwa makontena hayo.

Kwa upande wake Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam, Njaule Mdendu alisema kuwa ziara ya Waziri imetoa mwanga mpya katika kusimamia usafirishaji wa chuma chakavu na kuahidi kufanyia kazi changamoto zake..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles