29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Simba atamba kuimaliza UD Songo Taifa

MWAMVITA MTANDA, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba,  Patrick Aussems , amesema anaamini kikosi chake kitatumia vizuri ardhi ya nyumbani kuiondosha mashindanoni UD Songo na kutinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba juzi ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya UD Songo ya Msumbuji, katika mchezo  wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Jiji la Kibiashara la Beira, Msumbiji.

Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo, utachezwa  Agosti 25 mwaka huu,   Uwanja wa taifa,  Jijini Dar es Salaam.

Ili kusonga mbele, Simba inahitaji ushindi tu, tofauti na wapinzani wao ambao matokeo ya sare ya mabao yoyote yatawabeba kwa kuzingatia kigezo cha bao la ugenini.

Akizungumza na MTANZANIA  jana, Aussems alisema,  walikusudia kupata ushindi ugenini, lakini wakakwama na sasa wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani.

Alisema,  amewasoma vizuri wapinzani wao na kubaini kasoro kadhaa ambazo ana amini watazitumia kupata ushindi katika mchezo wa marudiano.

“ Sina muda wa kupoteza tena ndio maana tumerudi na kuanza mazoezi haraka,  hii michuano ni migumu.

“Ili kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele tulipaswa kushinda ugenini na nyumbani. Jambo la kujivunia ni kwamba nyumbani tutacheza tukiwa na mashabiki wetu ambao wana maana kubwa katika kufanikisha ushindi wetu.

“Pia unaweza kuona mazingira ya uwanja tuliochezea mechi ugenini ni tofauti na Taifa ambao unaruhusu kuucheza mchezo wetu,”alisema Aussems.

Aussems  tofauti na msimu uliopita ambapo malengo yalikuwa kufika hatua ya makundi lakini wanafanikiwa kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, safari hii  wamejiandaa kwa mapambano ya kuwania ubingwa.
Kuhusu hali za wachezaji wake waliosafiri Msumbuji alisema wote wako timamu kimwili.

Raia huyo wa Ubelgiji alisema
watautumia mchezo wa Ngao ya jamii kuashiria msimu mpya wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuchezwa mkoani Iringa Agosti 17 mwaka huu kujipika kabla ya kuivaa UD Songo.

“Mipango ya sasa,  wachezaji hawatakuwa wanakaa majumbani kwao kwa muda mrefu, badala yake watakuwa kambini ili mawazo yao yaelekee kwenye majukumu waliyonayo,”alisema.

Wakati huo huo, kikosi cha Simba kimereja nchini na jana jioni kiliendelea na mazoezi  kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles