24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NEMC: Kelele za baa huathiri nguvu za kiume, mimba

CHRISTINA GAULUHANGA-Dar es Salaam

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema utafiti unaonesha kelele zaidi ya viwango husababisha upungufu wa nguvu za kiume, mimba kuharibika na kuleta athari za akili na afya ya ubongo.

Akizungumza jana Dar es Salaam na wamiliki wa baa, kumbi za starehe na sherehe kuhusu athari za kelele zilizo juu ya viwango vilivyoainishwa mwaka 2015 juu ya viwango vya udhibiti wa uchafuzi, kelele na mitetemo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Samuel Mafwenga, alisema tangu mwaka 2016 hadi 2019 wamepokea malalamiko 4,790 ambayo kati ya hayo 952 sawa na asilimia 20 ni ya kelele.

Mafwenga alisema tafiti zinaonesha kelele zina athari kwa watoto kiakili, kiafya na kwa wajawazito na wazee pia.

“Tafiti zinaonesha kelele zikizidi zaidi ya viwango zina athari ya faragha, hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kiume na kuwanyima watu faragha,” alisema Mafwenga.

Alisema tangu Januari mwaka huu hadi sasa amepokea malalamiko 200 ya kelele jambo ambalo linahitaji elimu zaidi ya uelewa juu ya athari za kelele.

“Kwa mwezi mmoja uliopita nimepokea malalamiko 100 ambayo naendelea kuyafanyia kazi, hivyo kelele ni kero na zina athari ndani ya jamii kiafya na kimazingira,” alisema Mafwenga.

Alisema ili kuondoa kero hiyo ndani ya jamii, ni vyema wamiliki wakatumia vifaa vya kupunguza kelele ili waweze kupima viwango vya kelele wanavyovizalisha.

Mafwenga alisema kelele hizo hazihusu nyumba za ibada kwakuwa ana imani ni walinda amani.

“Mambo ya kuzingatia katika kudhibiti ni muda wa kelele, ukaribu wa makazi ya watu, ukaribu wa ukanda wa kudhibiti kelele, kelele za kujirudia, vipindi au mfululizo na nyinginezo,” alisema Mafwenga.

Alitaja viwango vya kelele vinavyoruhusiwa vimegawanywa katika makundi ya kawaida, kelele zinazoendelea viwandani au karakana, kelele za mara moja eneo la ujenzi, kutangaza kwa kipaza sauti, kumbi za starehe, nyumba za ibada, magari, migodi na machimbo.

Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira, Dk. Ruth Lugwisha, alisema sheria hiyo inaanza kutekelezwa, hivyo ni vyema wadau wakaanza kuzingatia umuhimu wa vipima sauti.

Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Baa na Kumbi za Burudani Tanzania (Ubakuta), Potipoti Ndanga, alisema hawafahamu sheria zilizopo zimetungwa mwaka gani kwakuwa hakukuwa na ushirikishwaji wa wadau.

Alisema viwango vya faini na sheria iliyopo sasa ni lazima iangalie mazingira ya wadau wake ambao wanafanya jitihada za kuendeleza uchumi wa nchi na familia zao.

“Sheria zilizopo msije mkawa mmeweka kwa ajili ya kujaza matumbo ya watu, kwani angalieni mmetushirikishaje na viwango hivyo vya faini,” alisema Ndanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles