24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nehemia Mchechu mgeni rasmi tamasha la ‘mateja’

Nehemia MchechuNA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la kwaya mbalimbali lenye lengo la kuchangia uanzishwaji wa Kituo cha kusaidia vijana walioathirika na dawa za kulevya.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kigogo, litafanyika Jumapili ya Oktoba 18, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Msanii kutoka Kenya, Solomoni Mukubwa, kwaya ya Kijitonyama Uinjilisti, Kwaya Kuu ya KKKT Kijichi, Keko, Luguruni, Kwaya ya Umoja wa Akina mama Mabibo Farasi na nyingine nyingi zitaongoza katika nyimbo.

Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kigogo, Richard Hananja, alisema tamasha hilo limelenga kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha kusaidia vijana walioachana na dawa za kulevya na wameamua kumrudia Mungu.

Mchungaji huyo alisema, kituo hicho kitasaidia vijana kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro na Pwani katika mafunzo ya ufundi stadi, ujasiriamali pamoja na elimu ya kujitegemea ili waweze kuanzisha maisha yao.

Aliongeza kwamba, tiketi za tamasha hilo zinapatikana katika makanisa yote ya KKKT jijini Dar es Salaam, lakini pia michango kwa ajili ya huduma za kiroho inaweza kuwasilishwa kupitia namba 0719 083807 na 0752 445726.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles