23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Nedy Music na tabia za Ommy Dimpozi

Said Seif (Nedy Music)
Said Seif (Nedy Music)

NA MWANDISHI WETU,

SAID Seif ni mmoja wa wasanii wanaokuja vizuri katika muziki wa kizazi kipya ambaye jina lake maarufu ni Nedy Music.

Huyu ni msanii anayewakilisha kundi la Pose kwa Pose (PKP) linalomilikiwa na mkali wa mapozi, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

Wimbo wa ‘Usiende Mbali’ alioshirikiana na bosi wake, Ommy Dimpoz, ndio unaomtambulisha vema katika muziki wa kizazi kipya.

Msanii huyo ana ndoto na mwelekeo mkubwa kuwa kama bosi wake huyo kwa kuiga mambo yake mengi ikiwemo tabia kubwa ya kuficha uhusiano wake wa kimapenzi.

Neddy amekuwa akihisiwa kutoka kimapenzi na wasanii waliomzidi umri akiwemo Shilole anayedaiwa kuwa naye baada ya msanii huyo kuachana na aliyekuwa dogodogo wake, Nuh Mziwanda, lakini hadi leo anaendelea kukataa tuhuma hizo.

Kukataa kwake huko kunaonyesha namna anavyoiga njia alizopita bosi wake, Ommy Dimpozi ambaye hadi leo anaendelea kuleta utata juu ya uhusiano wake wa kimapenzi.

Kutokana na jambo hilo, mashabiki wa msanii huyo wameonyesha hisia kwamba msanii huyo anafuata nyayo za bosi wake kwa kutotaka kujulikana mpenzi wake ama kutokuwa naye kweli kama alivyo bosi wake huyo.

Jambo hilo pia linaweza kumletea sintofahamu nyingi hapo baadaye kiasi cha kuwaongezea nafasi waimbaji wa jamii ya Ney wa Mitego kuwaimba tofauti na wao wanavyojiweka.

Lakini yote kwa yote ni namna nzuri ya kuishi kama hakuna baya wala tatizo lolote kwao, pia msanii huyu anaiga namna ya mavazi anayovaa bosi wake na huwa na mwonekano mzuri na huvaa nadhifu ingawa si mtu wa kuchanganya mavazi mengi na yenye mwonekano tofauti kama bosi wake.

Jambo hilo ni zuri na la kuigwa na wasanii wengine kwa kuwa msanii anatakiwa awe na mwonekano nadhifu haijalishi wa muziki wa aina gani kama wafanyavyo wasanii wa baadhi ya makundi likiwemo kundi la Wasafi Classic linaloongozwa na msanii, Diamond Platnumz.

Nedy alipofanya mazungumzo na MTANZANIA ilikuwa kama ifuatavyo;

Mtanzania: Kwanini upo PKP na si lebo nyingine?

Nedy Music: Nilikuwa na ndoto na Ommy Dimpoz na yeye pia alikuwa na mawazo na mimi ndiyo maana nipo katika lebo yake.

Mtanzania: Vipi una mpenzi au huna kama Dimpoz?

Nedy Music: Mimi sina mpenzi kwa sasa bado mambo yangu hayajakaa sawa pia sijawaza kuwa na mpenzi kwa sasa.

Mtanzania: Vipi uliachana na Shilole?

Nedy Music: Shilole ni rafiki yangu na msanii wenzangu hakuna mapenzi kati yetu, pia haiwezekani kuwa naye amenizidi umri sana.

Mtanzania: Changamoto gani umepitia hadi leo katika muziki wako?

Nedy Music: Kukutana na Ommy ilichukua muda mrefu, pia marafiki walikuwa wakinikatisha tamaa kwamba sitaweza kufikia nilikofikia na pia mambo mengine ya kawaida.

Mtanzania: Ukiwa na tatizo nani wa kwanza kumwambia?

Nedy Music: Mama yangu ndiye mtu wa kwanza ambaye nikiwa na matatizo naweza kumwambia.

Mtanzania: Unazungumziaje kuchora tattoo na kutoboa masikio kwa wasanii?

Nedy Music: Sijachora tattoo wala sitachora mwilini mwangu wala kutoboa masikio, mimi si wa kuigaiga mambo labda nivae za kubandika tena wakati wa shoo.

Pia nawashauri wasanii wenzangu wanaochipukia wasikate tamaa hata wakatishwapo waamini kwamba ipo siku itafika watafanikiwa tu safari bado ndefu lakini tuombeane ili tufanikishe tunachokitafuta katika muziki na kuiwakilisha nchi yetu vizuri kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles