Ne-Yo afurahi kupata mtoto wa kiume

0
697

Ne-YoNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Shaffer Smith (Ne-Yo), amefurahishwa na mkewe, Crystal Renay, aliyefunga naye ndoa wiki iliyopita kwa kumpatia mtoto wa kiume.

“Ni furaha kuitwa baba, lakini furaha yangu kubwa ni kupata mtoto wa kiume, nilikuwa natamani muda mrefu na nashukuru Mungu imekuwa kama nilivyomuomba,” alisema Ne Yo.

Hata hivyo, msanii huyo kwa sasa ana jumla ya watoto watatu, wa kwanza wa kiume, Mason Evan wa pili wa kike, Madilyn Grace na huyu wa sasa ambaye ni wa kiume.

“Familia kwa sasa inakuwa kubwa, kilichobaki ni kutekeleza majukumu ya kuilea familia yangu, sitaki waje kuyumba maishani mwao,” aliongeza Ne-Yo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here