31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mtoto wa msanii awaliza watu Malawi

Grace-Chinga-MalawiLILONGWE, MALAWI

MTOTO wa marehemu, Grace Chinga, Miracle Chinga, juzi aliwaliza waombolezaji waliojitokeza katika mazishi ya msanii huyo baada ya mtoto huyo kuimba wimbo wa kumuaga mama yake.

Grace alikuwa msanii maarufu wa muziki wa Injili nchini humo, alifariki baada ya kusumbuliwa na maumivu makali ya kichwa. Mazishi yake yalifanyika juzi kwenye mji wa Blantyre.

Kabla ya mazishi hayo kufanyika mtoto wa marehemu ambaye anajulikana kwa jina la Miracle, aliomba kumuaga mama yake kwa wimbo ambao ulijulikana kwa jina la ‘Kwa heri Mama’.

Hata hivyo, wakati anaimba alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akibubujikwa machozi na kusababisha maelfu ya waombolezaji kudondosha machozi pia.

Zaidi ya watu 20,000 inadaiwa walijitokeza katika mazishi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles