28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NDUGAI: LISSU ANATIBIWA KWA MSAADA WA UJERUMANI


Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye yupo kwenye matibabu nchini Ubeligiji, anatibiwa kwa msaada wa Ubalozi wa Ujerumani.

Spika Ndugai amesema hayo wakati akitoa mwongozo aliiombwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema, (Chadema) ambaye alitaka kujua sababu za Mbunge huyo kutolipiwa matibabu yake na Serikali ilihali watu wengine akiwamo Spika amekuwa akilipiwa na Serikali.

 “Tunaendelea na vikao vya bajeti Mbunge mwenzetu Tundu Lissu yupo bado Hospitalini Ubelgiji na ofisi ya Spika bado imeendelea kukaa kumlipia matibabu yake nab ado ofisi ya Bunge na kama wewe mungu amekusaidia umerudi hivi karibuni Nchini ukitokea India kwa matibabu.

“Lakini Serikali imegharamia kila kitu chako leo Mbunge bado yupo Hospitali lakini Serikali haijaona wajibu inawezekana jambo hilo halijatokea jana lakini makusudi ya kutafuta upendo wako tunaomba ulitolee ufafanuzi.

“Kwanini wewe Serikali inawajibu wa  kugaramia matibabu yako lakiniMbunge aliyepigwa risasi Dodoma lakini Bunge  linashindwa kuwajibikia wajibu huo,”aliuliza.

Akijibu mwongozo huo, Spika Ndugai alisema, “utaratibu ni utaratibu na ni kwa watu wote, unaweza kwenda kutibiwa kwa kutumia njia binafsi ya umma ambayo ina taratibu zake, hata hivyo tunawashukuru Ubalozi wa Ujerumani ambao wanatibu Mheshimiwa Lisu kule Belgium alipo.

“Hili jambo (Lissu anayetibiwa Ubelgiji) aliniambia Balozi wa Ujerumani mwenyewe, tunashukuru pia kwa msaada huo  ambao tunaupata,” alisema Ndugai.

Ndugai pia amesema “bahati mbaya unaliweka moja kwa moja kwangu, ukitaka kujenga hoja, jenga moja kwa moja kwa sababu hakuna asiyestahilina na anayestahili.

“Nirudie tena nimekuwa sipendi sana swali hili kwa sababu wenzetu  yupo Hospitalini bado, lakini mnavyochokoza na mimi naweka kidogo kidogo.

“Nianze kusema kuna aina mbili ya kupatiwa matibabu kwa wabunge na wananchi wote, moja ni njia ya umma na pili Private.

“Wewe hukuwepo (wakati Lissu alipopirwa risasi) wakati wenzako walipoamua kumpeleka Nairobi  alikuwepo mwakilishi wa familia na viongozi wako Msigwa (Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa) na Kiongozi wa Kambi (Freeman Mbowe), ambao ni wajumbe wa kamisheni, ule wa kumpeleka  Nairobi ulikuwa uamuzi binafsi.

“Wapo wabunge wengi tu ambao wanaenda kwenye matibabu kwa njia binafsi sina haja ya kuwataja majina lakini ni wengi watani zangu kama Charles Kitwanga ambaye ameniaga anaenda kutibiwa Ujerumani,” alisema Ndugai.

Alisema kwa uratabu wa kupata matibabu nje ya nchi kwa mtu yeyote, lazima kuwe na Barua ya Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ikieleza rufaha hiyo inaenda hospitali gani nje ya nchi, Barua ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto pamoja na kibali cha Rais.

“Ninyi mlichagua Private root kwahiyo Mheshimiwa Lema wewe niletee tu barua ya Wizara ya Afya na ya Muhimbili hii ya Rais naweza kukusaidia,”

“Kwa hiyo hii ya fulani ni mambo ambayo hayana maana wala hakuna yeyote anayebaguliwa, asimame hapa mtu yeyote ambaye aliwahi kwenda kwa utaraibu huo halafu akakosa kutibiwa na fedha za uuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles