31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BAJETI YA AFYA YAFEKWA


 Fredy Azzah, Dodoma   |

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, imesema mpaka kufikia Februari mwaka huu, Serikali ilikuwa imetoa Sh bilioni 576.52 pekee kati ya Sh trilioni 1.07 zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18, huku bajeti ijayo ikiwa imepungua kwa Sh bilioni 171.6.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, akisoma maoni ya kamati yake baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kusoma makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara yake, alisema fedha hizo zilizotolewa ni asilimia 53 tu ja bajeti yote iliyopitishwa na Bunge.

Alisema pia kati ya fedha zilizotolewa, Sh bilioni 190.75 ni za matumizi ya kawaida ya wizara.

“Uchambuzi wa kamti umebaini fedha zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa shughuli wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18, ni kiasi kidogo amcho hakiridhishi na kinyume na matarajio ya Mpango wa Bajeti ambao Bunge na Serikali tulikubaliana,” alisema.

Kwa upande mwingine, bajeti ijayo ya wizara ya Afya imepungua kw Sh bilioni 171.6 ikilinganishwa na ile inayoishia Juni 30.

Akisoma hotuba bungeni jana, Waziri Mwalimu alisema kwa mwaka wa fedha ujao, wizara yake inaomba kuidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 898.374 ikilinganishwa na Sh trilioni 1.07.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles