27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai atajwa kesi ya ufisadi Ngorongoro

ndugai (1) NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ametajwa katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA),  upotevu  wa Dola za Marekani 66,890 sawa na Sh. Milioni 133.7

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mhifadhi Mkuu wa zamani wa NCAA, Benard Murunya ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Meneja wa Utalii wa NCAA Veronica Funguo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Cosmas ya Uwakala wa Usafirishaji Salha Issa.

Kesi hiyo iliendelea jana mahakamani hapa kwa shahidi wa kwanza wa Serikali ambaye ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa NCAA,Sezari Semfukwe kuhojiwa na Wakili wa utetezi Joseph Boniface mara baada ya kumaliza kutoa ushahidi.

Akihojiwa na Wakili Boniface, Shahidi alidai mbele ya Hakimu ya Patricia Kisinda wa Mahakama ya wilaya ya Arusha, kwa mujibu wa nyaraka Murunya aliithinisha malipo ya Dola za Marekani 66,890 kwa Kampuni ya Uwakala ya Cosmos ambayo haikufanya kazi husika.

Alidai kuwa malipo hayo yalikuwa kwa ajili ya Safari ya Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige, Murunya na Msaidizi wa Waziri Egidius Muyungi ambao hawakutumia tiketi za Kampuni ya Uwakala ya Cosmos.

Badala yake Aalidai malipo mengine kupitia hundi namba 310/0379 ya Oktoba 29, Mwaka 2011 na Tranformer Invoice namba 5609 ya Septemba 7, Mwaka 2011 yenye Dola za Marekani 66,890 yalilipwa kwa Antelope Tours& Traveling kwa tiketi ya Waziri Maige, Murunya, Muyungi na kusafiri kwenda Marekani.

“Baada ya kupata taarifa kuwa huduma haikutolewa Mhifadhi Mkuu aliandika barua ya kutaka kujiridhisha kama huduma ilitolewa na Kampuni ya Cosmas au haikutolewa,” alidai shahidi huyo wa Serikali ambaye ofisi yake inahusika na malipo na kumbukumbu zote za fedha.

Hata hivyo Wakili wa Utetezi Boniface alimpatia kusoma barua ya Mhifadhi Mkuu kwenda Kampuni ya Cosmas iliyokuwa ikionyesha malipo yalivyofanywa kwa kampuni hiyo lakini huduma haitolewa.

Katika hatua hiyo hiyo Wakili Bonaface alimpatia tena shahidi barua yenye majibu kutoka Kampuni ya Cosmas kwenda kwa Mhifadhi Mkuu ambapo shahidi aliisoma na kueleza kuwa, Kampuni ya Cosmas ilikiri kupokea fedha lakini haikutoa huduma.

Alidai kwa mujibu wa barua ya Kampuni ya Cosmas waliahidi kutoa tiketi nyingine kwa ajili ya safari Murunya, Naibu Spika Job Ndugai, Peter Makutiani, Machumu na Kamamba.

“Hawa walisafirishwa na Kampuni ya Uwakala ya Cosmas na hawana uhusiano na malipo ya awali,” alidai Shahidi aliyemaliza kutoa ushahidi wake jana akiongozwa na Wakili wa Hamidu Sembano anayesaidiana na Wakili Mwandamizi Rehema Mteta.

Awali mahakamani hapo Wakili wa Utetezi Boniface aliwasilisha ombi la kujitoa kumtetea mshitakiwa wa kwanza Murunya kutokana na kile alichodai kuwapo kwa mawasiliano hafifu baina yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles