29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ndege za JPM zaanza safari Mwanza-Dar

Abiria wakishuka kwenye ndege aina ya Bombardier Dash-8 Q 400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), iliyoanza safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza, juzi.
Abiria wakishuka kwenye ndege aina ya Bombardier Dash-8 Q 400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), iliyoanza safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza, juzi.

Na BENJAMIN MASESE,

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limezindua rasmi safari za ndege zake aina ya Bombardier Dash-8 Q 400 kati ya  Dar es Salaam  na Mwanza huku  viongozi wa Serikali wakiwataka Watanzania  kutanguliza uzalendo kwanza kwa kuthamini vitu vyao   kukuza uchumi wa shirika hilo.

Uzinduzi huo ulifanyika juzi  baada ya ndege hiyo kuwasili Mwanza kwa mara ya kwanza    saa 10.45 jioni  ikiwa na abiria zaidi ya 90 waliokuwa wamefuatana  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamriho na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella   wajumbe wa bodi ya  ATCL.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Chamriho alisema safari za ndege hizo kwenda Mwanza  ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Magufuli wakati wa kampeni na  kwamba ATCL itaendelea kuimaraika ikiwa Watanzania watatanguliza uzalendo kwa kupanda ndege hiyo.

Alisema   Serikali imetoa maelekezo kwa ATCL kuhakikisha inakuwa na ushindani na kampuni znyingine kwa kuweka bei nafuu inayoendana na kipato cha watanzania.

Chamriho  alisema  ununuzi wa  ndege nyingine zilizoahidiwa kuongezwa itategemea ufanisi  utakaokuwapo.

“Rais Magufuli amekusudia kurejesha heshima ya ATCL, sote tunajua kwamba Mwanza kuna vivutio vingine na ndiyo mkoa ambao unawarahisishia wageni kufika kwenye mbuga zetu za Serengeti.

“Tumefanya uchunguzi na kubaini wakazi wa Kanda ya Ziwa wana mwamko na usafiri angani, ndege zote zinazotoka huku na kwenda Dar es Salaam huwa zimejaza abiria.

“Huu ni uwekezaji sahihi nawaombeni bodi  na menejimenti ya ATCL hakikisheni mnazingatia ushindani unaekwenda sambamba na utendaji wenye maadili mema, tunajua kuna changamoto zimejitokeza za kuchelewa.

“Zifanyieni kazi haraka, toeni vinywaji kwa abiria na kauli za ukarimu  kupata wateja wengi.

“Naomba niseme kwamba baada ya wiki moja ndege hizo zitafanya safari kati ya Mwanza na Bukoba, Tabora na Kigoma na tutakuwa tunaongeza safari nyingine kulingana na mahitaji lakini kikubwa nasisitiza mapato yadhibitiwe yasipotee kupitia mikono ya wachache,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles