24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wavuvi walalamikia Sumatra kutotoa stakabadhi za EFDs

mitumbwi

Na AHMED MAKONGO,

WAVUVI   katika  Kijiji cha Murangi, Majita, Musoma vijijini   wanaoendesha shughuli zao za uvuvi katika Ziwa Victoria, wamelalamikia kitendo cha Mamlaka ya Udhibiti wa Usafari wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA), kuwalipisha fedha za leseni ya mitumbwi yao kwa kutumia risiti za mkono, badala ya mashine za elektroniki (EFDs).

Waliyasema hayo baada ya maofisa wa Sumatra   kudai kila mtumbwi ulipiwe Sh  75,000, huku wakitoa risti za mkono bila kutumia mashine hizo.

Kwa mujibu wa wavuvi hao,  wao hawakatai kulipia leseni hizo bali kinachowashangaza ni   maofisa hao kuwalipisha kwa kutumia risti za mikono.

Walisema   wanapokataa kulipia leseni kwa utaratibu huo wa risiti za mikono maofisa hao wa Sumatra wamekuwa wakiwachukulia zana zao za uvuvi na kwenda nazo ofisini kwao.

Miaka mitatu iliyopita walilipia leseni zao na kupewa risti za mikono, lakini juzi maofisa hao wa Sumatra  walisema kuwa hizo risiti siyo za kwao na wakadaiwa   walipe upya, walisema wavuvi hao.

Waliiomba serikali kuingilia kati   suala hilo kwa vile inawezekana  kukawa na udanganifu kuhusu ukusanyaji huo wa kodi ya serikali.

“Sisi hatukatai kulipa leseni zetu maana hiyo ni kodi ya serikali, ila tunachoomba sisi wavuvi hao maofisa wawe na hizo mashine kama serikali ilivyokwisha kuagiza.

“Maana hali hii inatufanya kutokuwa na imani  kama kweli hawa ni maofisa wa Sumatra au siyo, maana sasa hivi matapeli ni wengi,” alisema mvuvi mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini.

Walisema kuwa   walikwisha kumpigia simu Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Vicent Naano, kuhusu suala hilo ambaye aliwaambia  wasikubali kutoa fedha kama hakuna mashine hizo za EFDs.

Ofisa wa Sumatra katika Mkoa wa Mara, Halma Lutavi, alipoulizwa   alisema  maofisa hao wa Sumatra wanafanya kazi kulinga na taratibu na sheria za nchi.

Alisema  wanatumia utaratibu huo wa njia ya mkono na kisha risti hizo kuziingiza kwenye mashine hizo ambazo ni kubwa na ziko ofisini.

Aliwaomba wananchi kuwaamini maofisa hao maana wanapofika kwenye maeneo yao huwa na vitamblisho vya kazi na pia ujitambulisha kwa uongozi wa eneo husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles