21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ndanda Kosovo kuzikwa leo Dar

ndandaNA MWALI IBRAHIM

MAZISHI ya aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini mwenye uraia wa Congo, Ndanda Kosovo, yanatarajia kufanyika leo kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Agizo hilo la kufanyika kwa mazishi hayo hapa nchini, limetolewa na mama yake mzazi aliyetoka Congo kuja kushiriki mazishi ya mwanawe huyo.

Mjomba wa marehemu huyo, Kadinal Gento, alisema familia imeruhusu taratibu zote za mazishi zifanyike hapa nchini ili kutoa nafasi kwa rafiki na watu wa karibu wa msanii huyo kushiriki mazishi hayo tofauti na yangefanyika nchini Congo.

“Kutokana na agizo hilo, kesho (leo), tutamsitiri mpendwa wetu kwenye makaburi ya Kinondoni ndugu, jamaa na marafiki pamoja na mashabiki wake wajumuike nasi katika safari ya mwisho ya ndugu yetu huyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles