24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ndama afikishwa mahakamani kwa kutakatisha fedha

avocat-drept-civil

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA Ndama Hussein maarufu ‘mtoto wa ng’ombe’ jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka sita likiwamo la kughushi na kutakatisha Dola za Marekani 540,390 (Sh bilioni 1.181).

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitakatisha fedha hizo zilizopatikana kwa njia ya jinai, kwa kuelekeza kiasi hicho cha fedha kuingizwa katika akaunti iliyopo benki ya Stanbic yenye jina la Kampuni ya Muru Platnum.

Ilidaiwa kuwa  baadaye alizitoa zote na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi huku akijua zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa akisaidiana na Wakili wa Serikali, Leonard Challo.

Msigwa alidai kuwa Februari 20, mwaka 2014,  Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na lengo la kudanganya alighushi nyaraka za kusafirisha madini.

Alidai mshitakiwa alionyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited imepewa kibali cha kusafirisha makasha manne ya vipande wa dhahabu ya uzito wa kilo 207 na thamani ya Dola za Marekani 8.2 kwa Kampuni yenye makazi yake Australia ya Trade TJL DTYL Limited huku akijua nyaraka hizo niza uongo.

Katika shtaka la pili, Machi 6, mwaka 2014,  Dar es Salaam akiwa na nia ya kudanganya, aliandaa nyaraka za uongo kuonyesha kwamba hati ya kuondolea mizigo kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa za tarehe hiyo, akiwa na lengo la kuonyesha kwamba vipande vya dhahabu vyenye uzito wa kilo 207 kutoka Jamhuri ya Congo, kuwa zinasafirishwa na Kampuni ya  Muru Platnum kwenda Australia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles