24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Maiti yagombewa, yakwama kuzikwa kwa siku 10

coffin2_2-jpgb9394da4-5103-4409-9c3b-07fbc28eeaf1original

Na Kulwa Mzee -Dar es Salaam

MWILI wa marehemu Ernest Materego, aliyefariki Dar es Salaam Novemba 19, mwaka huu, umekwama kuzikwa kwa zaidi ya siku 10 kutokana na kuibuka mgogoro wa wapi uzikwe.

Mgogoro huo umeibuka baada ya mdogo wa marehemu, mke na mtoto kuzozana hadi kufungua kesi mahakamani ili kupata mwafaka wa mahali mwili huo utakapozikwa kati ya Dar es Salaam na Bunda mkoani Mara.

Kesi hiyo ya madai inasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wadai katika kesi hiyo ni Joyce Materego (mke wa marehemu) na Edwin Materego (mtoto wa marehemu) wanaowakilishwa na Wakili Raymond Wawa wakati mdaiwa ni Gonche Materego (mdogo wa marehemu) ambaye anawakilishwa na Wakili Makaki Masatu.

Wadai wanadai kuwa walitaka kuzika Dar es Salaam kwa sababu ndiko marehemu aliishi wakati wa uhai wake tangu mwaka 1974.

Mdaiwa akijibu madai hayo, alidai marehemu alikuwa akiishi pia Bunda wakati wa uhai wake, hivyo anatakiwa kuzikwa huko na si Dar es Salaam.

Wadai waliomba mahakama itoe amri ya muda mwili huo kutozikwa hadi kesi hiyo imalizike na ikakubali.

Hata hivyo, wakati amri hiyo inatolewa, mwili wa marehemu ulikuwa njiani kusafirishwa kuelekea Bunda, hivyo waliamriwa wasizike badala yake wahifadhi mwili katika hospitali mahali watakaposimama hadi shauri litakapomalizika.

Wakili wa mdaiwa, Masatu aliwasilisha pingamizi mahakamani akidai mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo kwa sababu inahusu masuala ya kimila, hivyo ifutwe.

Akijibu hoja hiyo, wakili wa wadai, Wawa, alidai kuwa hoja iliyopo mahakamani si suala la kimila, bali wapi mwili wa marehemu ukazikwe.

Wawa alipingana na hoja za wadaiwa na kudai kwamba mahakama hiyo ina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Simba alisema atatoa uamuzi leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles