25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ndalichako:Taifa linahitaji mafundi sanifu

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amesema Taifa lina mahitaji makubwa ya mafundi sanifu na amewataka wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam wakadumishe weledi na kasi ya kufanya kazi kwa kiwango cha juu.

Waziri alisema hayo katika mahafali ya 12 ya taasisi hiyo wakati akiwatunukia shahada na stashahada mbalimbali wahitimu 774.

Aliwataka wahitimu wakazingatie maadili kwani Serikali haiwavumilii watu wazembe, kila mmoja afanye kazi kwa bidii na ubunifu.

“Dumisheni amani, umoja, mshikamano, daima msikubali kutumika kuligawa Taifa,” alisema.

Waziri Ndalichako alitoa wito kwa wahitimu hao wasiishie kutengeneza vitu vya ubunifu vya mifano, anataka vionekane sokoni, vitumike kwa matumizi ya jamii.

 Aliwashauri watengeneze zana za kilimo pia kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo.

“Bunifu zenu ziingie mtaani kama taa za kuongozea magari mlizobuni, zinafanya kazi vizuri, zimefungwa Dar es Salaam, Zanzibar,Simiyu, Mwanza na Musoma.

“Kumbukeni mafanikio yenu yatategemea namna gani mtatumia ujuzi mliopata, changamoto haziwezi kukosekana lakini lazima muwe nauthubutu,” alisema.

Alisema Serikali inatambua changamoto walizokuwa nazo na inaimarisha elimu na stadi mbalimbali za ufundi ikiwemo na vyuo vya ufundi sanifu.

Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Preksedis Ndomba,akizungumza katika mahafali hayo, alisema wanaandaa wahitimu wanaokwenda kujitegemea.

Alisema wapo wanaotaka kuanzisha viwanda wanahangaika wabuni kitu gani, anawashauri wafike DIT kuna bunifu nyingi ikiwemo hiyo ya taa za kuongozea magari barabarani wanaweza kuchukua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles