28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

NCCR yataka Rugemalila apelekwe mahakamani

Pg 3Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimeitaka Serikali kuwawajibisha wahusika wakuu walioshiriki katika uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow wakiwamo waliotoa rushwa ili kufanikisha mchakato huo.
Akizungumza katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Mosena Nyambabe, alisema Serikali imepeleka mahakamani maofisa wa ngazi za chini waliohusika katika sakata hilo na kuwaacha watu muhimu waliotoa rushwa.
“Mtuhumiwa namba moja ni mtu aliyetoa rushwa, lakini chakushangaza maofisa wadogo ndio wanaofikishwa mahakamani pekee, Serikali iseme huyu ambaye alihusika kugawa hizo fedha atapelekwa lini mahakamani,”alisema Nyambabe.
Alisema hatua za kisheria pia zinapaswa kuchukuliwa kwa wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge pamoja na waliohusika katika mgawo huo kwakuwa kuwajibika kisiasa kwa kujiuzulu katika nyadhifa zao pekee haitoshi.
“NCCR tunataka kujua kwanini baadhi ya waliopokea rushwa kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow kupitia akaunti ya Mkombozi wamefikishwa mahakamani,lakini watu wengine kama Profesa Tibaijuka, Chenge, Ngeleja na wengine hawafikishwi mahakamani,”alisema Nyambabe.
Alisema Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) imekuwa ikificha maovu likiwamo sakata hilo ambalo walikuwa wanalijua mapema na kusubiri vyama vya upinzani walikomalie.
Kuhusu mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa mwishoni mwa wiki na Rais Jakaya Kikwete, alisema rais alipaswa kuteua watu wapya wenye uwezo badala ya kuwarudisha mawaziri ambao walikwishatajwa kuwa mizigo.
“Ni mara ya saba sasa rais anabadilisha Baraza la Mawaziri, imekuwa kama mazoea mtu akiharibu anapelekwa sehemu nyingine,tunaweza kufananisha mabadiliko haya sawa na maigizo,”alisema Nyambabe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles