27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

NCCR-Mageuzi kuipeleka IPTL kwa wananchi

GRACE SHITUNDU NA NEEMA BARIKI (TSJ)

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimetangaza kulipeleka sakata la IPTL kwa wananchi na kutoa elimu kwao namna suala hilo lilivyozimwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Chama hicho kimesema kinatarajia kuanza ziara mkoani Kigoma wiki ijayo, huku ajenda kubwa ikiwa ni sakata la IPTL.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosen

David Kafulila
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila

a Nyababe, alisema chama hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kuona Serikali haioni umuhimu na uzito wa wizi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa juu.

“Hatujaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali juu ya suala hili, hivyo tunafanya utaratibu wa kuwasiliana na vyama ndani ya Ukawa kuona namna bora ya kulisukuma suala hili, ili Watanzania waelewe jinsi nchi yao inavyotafunwa.

“Pia tunaviomba hata vyama vilivyo nje ya Ukawa kulitambua suala hili na kulichukulia ni la wote na si la Kafulila au NCCR peke yake. Tunaamini fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Escrow zinalengwa kutumika kwenye harakati za uchaguzi mkuu ujao,” alisema Nyambabe.

Katibu Mkuu huyo wa NCCR-Mageuzi alisema kutokana na uzito unaochukuliwa sasa, hakuna dalili ya jambo hilo kupewa umuhimu, licha ya kuamuliwa lichunguzwe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Alisema ukweli kuhusu suala hilo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitakiwa kuunda kamati teule ambayo ingeweza kutoa majibu ya kweli kuhusu wizi huo.

“Ni aibu kwa Spika kukataa Bunge lisichukue jukumu lake la kuichunguza Serikali. Wote tunafahamu CAG alivyomsafisha Jairo au Takukuru ilivyosafisha Richmond.

“Ni katika msingi huo kama chama tunashauri suala hili linalogusa vigogo wakubwa nchini lichunguzwe na Bunge lenyewe au uchunguzi ufanywe na kampuni za kimataifa za ukaguzi kama ilivyofanyika kwenye fedha za EPA,” alisema.

Akizungumzia suala la usalama wa Kafulila, alisema endapo jambo lolote baya litamtokea mbunge huyo, NCCR Mageuzi inajua wanaohusika ni baadhi ya watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakitoa vitisho kila kukicha kwa mbunge huyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, alisema katu hatorudi nyuma licha ya kupokea vitisho.

“Sitaogopa lolote, nitaendelea kusema kweli na sasa ninaandika kitabu kitakachoeleza ufisadi huu na ninamuomba Mungu kabla kichwa hakijakatwa niwe nimekimaliza,” alisema Kafulila.

Juni 26, mwaka huu, Kafulila aliingia katika mapambano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, ambaye alimfananisha mbunge huyo na tumbili.

Kutokana na kauli hiyo, naye Kafulila alijibu mapigo kwa kumwita Jaji Werema mwizi kwa kumtaka atangaze maslahi katika sakata la uchotwaji wa Sh bilioni 200 katika akaunti ya Escrow.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

    • Ushauri wako unaenda sambamba na ule Spika wa Bunge Wizi/ufisadi ni jinai, sio masuala ya siasa ya kujitafutia sifa. Kafulila na Wenzake kama kweli mnao ushahidi malamiko yenu yapelekeni TAKUKURU/CAG mkamilishe ushahidi wahusika wafikishwe Mahakamani haki itendeke na ionakane na sio kuandamana. Kafulila alipofukuzwa NCCR alijua wapi haki iatafutwa, sio kwa mandamano ila kwenda mahakamani ili haki itendeke kisheia, iweje leo awadanganye vijana kutafuta haki kupitia Maandamano??!!.Vijana Chungeni sana hizi siasa za maji taka mtaumia, nawakumbusha Mahakama ilikwisha lidhia tamko la anayekaidi amri halali apigwe.

  1. Namwelewa Kafulila vema, unajua serikali ya CCM, haiwezi kuwajibika mahakamani, bali mahakama ya wananchi. Tazama jinsi Kikwete aliwafukuza kazi mawaziri mara mbili ni kwa sababu ya mahakama ya wananchi, ina nguvu sana kuliko mahakama zetu zilizojaa Rushwa nyingi. Dawa ni hiyo tu, halafu anaogopa kile kinachoitwa ” Usipeleke kesi ya ngedere kwa nyani au tumbili , kwani ni wale wale, haki haiwezi kutendeka kamwe.” Tanzania tunaijua, je ni kesi ngapi mahakama au polisi wameshughilikia, waache aende huko huko kwa wananchi. Kafulila songa mbele ukimaliza huko basi wapelekee ushahidi wako. Ukawa walipoondoka CCM na mashabiki wao walikuwa wanapiga kelele hizo hizo, kwamba Katiba haipatikani barabarani, leo je, wananchi wamewaelelwa Ukawa na hata viongozi wa dini wameelewa, kwamba uchakachuaji ni marufuku namna nyingine CCM hakuna kura Mwakani, chezea madhehebu ya dini wewe. ” Mungu haiwezi kudharauliwa na mwanadamu.” Soma biblia vizuri uone wafalme na watawala waliokuwa na kiburi walivyoadhibiwa na Mkono wa Mungu. CCM ni afadhali leo msingeiifanya migumu mioyo yenu (Zaburi 95:9)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles