25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ulipaji fidia ya ardhi wamtesa Tibaijuka

Profesa Anna Tibaijuka
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Na Aziza Masoud, Dar es Salaam

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amesema ingawa Serikali inapanga miji, bado inakabiliwa na changamoto ya kulipa fidia kwa wananchi inayotokana na ufinyu wa bajeti.

Profesa Tibaijuka aliyasema hayo alipotembelea banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana.

Alisema suala la fidia limeendelea kuwa changamoto kubwa katika miradi kutokana na ufinyu wa bajeti.

“Bajeti ya fidia zetu inategemea upatikanaji wa fedha ili tuweze kulipa fidia ya uhakika…viwango vya fidia ni endelevu na hiyo ndiyo changamoto tuliyonayo,” alisema.

Alisema katika kupanga miji, lazima watu wasumbuke hivyo wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo.

Wahandisi wanapaswa kuwa wakali katika ujenzi wa nyumba na kuhakikisha zinajengwa kwa viwango, ikizingatiwa ujenzi holela unahatarisha maisha ya watu, alisema.

“Nyumba ikijengwa kwa viwango inakaa hadi miaka 100, majengo yaliyojengwa chini ya kiwango ni hatari zaidi, watu wanaweza wakaangukiwa baada ya kuhamia,” alisema Tibaijuka.

Aliwataka wananchi kujitokeza kununua nyumba zinazojengwa na NHC ili mapato yatakayopatikana yawezeshe kujenga nyumba nyingine.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Felix Maagi, alisema shirika liko katika mikakati ya kujenga nyumba za kada zote kuanzia kipato cha chini mpaka cha juu.

“Hizi nyumba zitajengwa nchi nzima, ifikapo Desemba tutakuwa tumefika mikoa yote, lengo ni kuendelea kuboresha mazingira ya miji,” alisema Maagi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles