25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

NBA iwe mwalimu wa pili kwa  wachezaji wa kikapu Tanzania

NA GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

MSIMU mpya wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), umeanza rasmi na tayari michezo mbalimbali inaendelea kwa timu shiriki kuonyesha ubabe wao wa kuchukua ubingwa msimu huu.

Ukanda wa Mashariki zinashuhudiwa timu kama Atlanta Hawks, Boston Celtics, Charlotte Bobcats, Chicago Bulls, Cleveland Cavaliers, Detroit Pistons, Indiana Pacers, Miami Heat, Milwaukee Bucks, New Jersey Nets, New York Kinks, Orlando Magic, Philadelphia 76ers, Toronto Raptors na Washington Wizards

Kwa upande wa Magharibi ni Dallas Mavericks, Denver Nuggets, Golden State Warriors, Houston Rockets, Los Angeles Clippers,  Los Angeles Lakers na Memphis Grizzlies

Nyingine ni Minnesota Timberwolves, New Orleans Hornet, Oklahoma City Thunder, Phoenix Suns, Portland Trails Blazers, Sacramento Kings San Antonio Spurs Utah Jazz.

SPOTIKIKI lilipata nafasi ya kufanya mahojiano na viongozi, wachezaji wa timu za Tanzania kuhusiana na ligi hiyo, ambapo kila mmoja kwa mtazamo wake aliweza kuzungumzia na kutoa utabiri wake.

Michael Mwita (Katibu Mkuu TBF)

Ligi kikapu ya NBA ipo kwenye ‘pre season’ kwa sasa, ambapo timu ya Lakers inapewa nafasi ya kurudi katika makali yake, baada ya kufanya usajili mzuri, hivyo wanaweza kucheza fainali ya mwaka huu na Western kama watapita.

Anasema kwa hapa nyumbani, wachezaji wengi watakuwa wanajifunza zaidi mbinu za ushindi na watakuwa wafuatiliaji sana, hasa kwa timu kama Lakers, Golden State’s Warriors, Huston Portland kwa upande wa Mashariki.

Kwa upande wa Magharibi timu zitakazoangaliwa sana ni Boston Celtic, Piston Miluwakee, Bucks, Indiana pacers na Washington wizard zinatabiriwa kuwa wababe wa kanda hiyo, lakini Boston wananafasi kubwa ya kucheza fainali mwaka huu na Lakers au Huston au Golden State warriors

“Kwa wachezaji wetu moto utaongezeka sana na ligi yetu itakuwa ngumu sana hii ya NBL kufuatia kila mtu anataka kuwa kama mchezaji wa timu hizo zinazoshiriki katika ligi hiyo,” anasema Mwita.

Amini Mkosa (Naodha Savio)

Anasema ushindi anaipa Cavaliers, kwani ni timu ambayo inajituma na inaonyesha matumaini ya kuchukua ubingwa, mbali na kupoteza mwaka jana kwa kuzidiana pointi kwa kupokonywa na Golden State Warriors, msimu huu wameonyesha kujipanga ipasavyo watashinda.

“Timu nilizozitaja hapo juu zinauwezekano mkubwa wa kuingia fainali, muhimu ni ubora na kiwango chao, hili linaweza kuwa somo kwa wachezaji wa Tanzania, wanatakiwa kujifunza mambo mengi ikiwamo mbinu mbalimbali wanazotumia ili kushinda michezo yao wanayocheza.

“Tunaelekea katika michuano ya NBL, ukiwa kama mchezaji lazima uangalie wenzako wanafanya nini mpaka kufikia hapo walipo, tunajifunza mengi na ninaamini michuano hii itakuwa na ushindani wa hali ya juu,” anasema Mkosa.

Kablola Shomari ‘KB’ (Kocha)

Ni kocha wa timu ya Jogoo, anasema NBA ni michuano yenye ushindani mkubwa kwa kila timu kutafuta ushindi kwa udi na uvumba, msisimuko uliopo katika michuano kama hiyo husababisha mashabiki kujitokeza kwa wingi na pia wadhamini kujitokeza kwaajili ya kusapoti timu hizo.

“Ni michuano ambayo imeteka watu mbalimbali hata nchi za Afrika zinafuatilia michuano hiyo, tunaona kuwa serikali nayo inajitoa hasa kujenga viwanja vizuri,” anasema

Anasema timu ya Washington Wizard na Golden State Warriors kwa msimu huu zinaweza kukutana fainali,Warrior wakawa mabingwa mara ya pili mfululizo, baada ya kushinda tena mwaka jana.

Shamari anasema kwa upande wa wachezaji, NBA inaweza kuwa njia moja ya kuwasaidia kujifunza na vizuri ukiwa mchezaji  ujifunze kwa wenzako, wanafanya nini na wanatumia mbinu gani hapa ndipo unaweza kuwa mchezaji bora.

Erick John (Naodha Oilers)

Anasema michuano ya NBA inaleta msisimuko kutokana na wadhamini wengi kujitokeza katika kusapoti timu hizo.

Anasema pia serikali ya Marekani imeona umuhimu wa mchezo huo na imejenga viwanja vya kutosha ili kukuza na kuendeleza mchezo huo, tofauti na hapa nchini.

Anasema ubingwa anaipa timu ya Golden State Warriors kwa sababu ni timu ambayo wachezaji wake wanajituna na wanacharika kwa pamoja kufikia yale malemgo wanayotaka.

Okare Emesi (Mwenyekiti BD )

Mwenyekiti chama cha  Mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD), anasema michuano hiyo inawapa changamoto kubwa kujua nini wafanye ili waweze kufikia kama wao.

Anasema uwezekano wa Tanzania kufika mbali katika mchezo huo ni mkubwa, endapo serikali na wadau wakijitokeza na kuwekeza moja kwa moja kwa kujenga viwanja.

“Huston Portland wananafasi kubwa ya  kuchukua ubingwa endapo wachezaji wataongeza juhudi na kujituma kadri ya uwezo wao,”anasema Emesi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles