25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nauli mabasi ya mwendo kasi Sh1,200

mwendo kasiNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya UDA-RT imependekeza nauli kubwa itakayotozwa na mabasi ya mwendo kasi, ambayo imezua malalamiko Mapendekezo hayo yanaonesha kuwa nauli itakuwa Sh 1,200 kwa safari za njia kuu, Sh 700 njia za pembeni na Sh 1,400 njia kuu pamoja na njia ya pembeni, huku wanafunzi wakitakiwa kulipa nusu nauli ya mtu mzima.

Hata hivyo nauli hizo zimepingwa na kwamba mjadala mkali unatarajiwa kuibuka leo, wakati Mamlaka ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),itakapokutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusu nauli mpya iliyopendekezwa na kampuni hiyo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema sheria ya mamlaka hiyo, inaitaka kukusanya maoni kutoka kwa wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia kupanda kwa nauli.

“Kabla ya kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa, ikiwemo nauli za mabasi ni lazima mamlaka hiyo ikusanye maoni kutoka kwa wadau,” ilisema taarifa hiyo.

Katika kutekeleza hilo, mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau, watoa huduma, watumiaji wa huduma ikiwa ni pamoja na wananchi kwa ujumla.

Taarifa hiyo, ilisema mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 3.30 asubuhi na kwamba maoni yanaweza kutumwa kwa barua pepe, ikiwa ni pamoja na maandishi ambayo yanatakiwa kutumwa kabla ya Januari 13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles