Christopher Msekena
KAMPUNI kubwa ya muziki kutoka Jamaica, Natural Bond Entertainment, wameweka wazi mpango wa kukuza muziki wa Afrika kwa kuanza kushiriki kwenye albamu, Unity ya Buffalo Souljah, staa wa muziki Afrika Kusini mwenye asili ya Zimbabwe.
Prodyuza wa lebo hiyo Jarome Elvie, ameliambia MTANZANIA kuwa katika albamu ya Buffalo Souljah yenye jumla ya nyimbo 23, Natural Bond Entertainment wametengeneza ngoma mbili ambazo ni Family aliomshirikisha Starface na No Man Bigger Than God.
“Tumemchagua King wa African Dancehall, Buffalo Souljah ambaye pia anafanya Riddim na Reggae. Lengo la Natural Bond Entertainment ni kukuza muziki wa Afrika, tumeanza kufanya kazi kwenye albamu inayoitwa Unity ya Buffalo Souljah kwa kutengeneza nyimbo mbili ambazo tunaamini zitafanya vizuri pia mashabiki wanaweza kufuatilia kazi zetu kwenye Instagram tunatumia @naturalbondent,” alisema Elvie.