27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

NASA YATAJA POLISI INAODAI WALIVAMIA KITUO CHAO

NAIROBI, KENYA

MUUNGANO wa upinzani wa NASA juzi ulitaja majina ya maafisa wa polisi wanaodaiwa kuvamia kituo chao cha kuhesabia kura kilichopo mtaa wa Westlands mjini hapa.

Wakati wa mkutano wa mwisho wa NASA katika Bustani ya Uhuru, Seneta James Orengo alisema maafisa walioshambulia kituo hicho walikuwa 15.

Seneta huyo alitaja majina ya maafisa watano pekee na kuahidi kutoa ushahidi zaidi kwa wanahabari.

Hata hivyo, magazeti hayakuweza kuchapisha majina hayo kwa sababu za kisheria.

Licha ya seneta huyo kudai NASA iliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Parklands, Idara ya Polisi ilikana kupokea taarifa hiyo.

Katika taarifa, Msemaji wa Idara ya Polisi George Kinoti alikanusha madai ya kuhusika kwa polisi katika uvamizi na kuahidi kufanya uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles