23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

RIPOTI: ROBO YA VITUO VYA KUPIGA KURA HAVINA MAWASILIANO

NAIROBI, KENYA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imetangaza kuwa robo ya vituo vyote vya kupigia kura nchini hapa havina huduma nzuri ya mtandao wa simu wenye kasi wa 3G au 4G.

Tume imesema maafisa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo hivyo watalazimika kusogea hadi maeneo yenye huduma nzuri ya mtandao ndipo waweze kurusha matokeo.

Taarifa ya tume hiyo inasema kuna jumla ya vituo 11,155, ambavyo havina huduma nzuri ya mtandao wa 3G kati ya jumla ya vituo 40,883 kote nchini humo.

“Maafisa wasimamizi wa uchaguzi watatafuta mahala penye huduma nzuri ya mtandao au watumie simu za setelaiti kurusha matokeo,” tume hiyo imeandika kwenye Twitter.

Vituo hivyo visivyo na huduma nzuri ya simu vinapatikana katika kaunti 45 kote nchini humo.

Ni kaunti za Nairobi na Mombasa pekee ambazo hazijakumbwa na tatizo hilo.

Takwimu kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya zinaonesha maeneo mengi nje ya miji nchini humo hayana huduma ya 3G.

Ripoti kuhusu huduma ya simu na mtandao nchini Kenya ya mwaka jana inaonesha huduma ya 3G inapatikana kwa asilimia 17 pekee ya ardhi ya Kenya.

Hata hivyo, tofauti katika wingi wa watu maeneo mbalimbali, huduma hiyo huweza kufikia asilimia 78 ya wananchi nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles