Maregesi Paul, Dodoma
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), ameishauri serikali kuiondoa bungeni Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ili ikajipange upya na kuiboresha bajeti hiyo.
Pia amesema bajeti hiyo haina uhusiano wowote na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nape amesema hayo bungeni leo Mei 16, jijini Dodoma, alipokuwa akichangia bajeti ya wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19 iliyowasilishwa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.
“Tatizo kubwa linaloikabili serikali ni kuwekeza fedha nyingi katika miradi mikubwa inayoweza kujiendesha yenyewe badala ya kuwekeza katika maeneo yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi,” amesema Nape.
Hata hivyo, Nape alihoji mahali zinakopelekwa fedha wakati serikali inabana matumizi na kukusanya fedha nyingi.