23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Nani ni nani tuzo za AEAUSA2020

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Usiku wa kuamkia leo Jumatatu Desemba 21, limefanyika tukio kubwa la utoaji tuzo nchini Marekani za African Entertainment Awards USA (AEAUSA2020).

Katika tuzo hizo wasanii watatu wa muziki wa Bongo Fleva kutoka nchini Tanzania, Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz,’ Raymond Mwakyusa, ‘Rayvanny’ na Faustina Mfinanga, ‘Nandy’ wamefanikiwa kushinda tuzo hizo kwenye vipengele tofauti tofauti.

Mbali na Diamond Rayvanny na Nandy kushinda tuzo pia DJ Sinyorita kutoka Clouds Fm amefanikiwa kushinda tuzo ya DJ bora.

Diamond ametangazwa mshindi tuzo za aeausa 2020 katika kipengele cha (Msanii Bora wa Kiume) akiwashinda Eddy Kenzo, Wiz Kid , Shatta Wale, Stonebwoy, Davido, Burna Boy, Mohamed Abbas, Fally Ipupa na Jahllano ambao alikuwa akichuana nao kwenye Kipengele hicho.

Huku Rayvanny akitangazwa mshindi tuzo za Aeausa 2020 katika kipengele cha Best Male Artist – East/South and North Africa akiwashinda, Elgrande toto, The Ben, Diamond Platnumz, Alikiba, Eddy Kenzo, Harmonize, Tewodros kassahun aka Teddy Afro, Jah Prayzah na Bruce Melodie.

Kwa upande wa Nandy ametangazwa mshindi tuzo za Aeausa 2020 katika kipengele cha “Best Female Artist” akiwashinda Zahara, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sho Madjozi, Sha Sha, Sheebah Karungi, Rema Namakula, Aya Nakamura na Kenza Morsli.

DJ pekee kutoka Tanzania DJ Sinyorita ameshinda kipengelea cha DJ bora akiwashinda DJ Moh

  1. DJ Cuppy
  2. DJ Slick Stuart & DJ Roja
  3. DJ Shimza
  4. DJ Nelasta
  5. DJ Tunez
  6. DJ Xclusive
  7. DJ K Meta
  8. DJ Roma

Orodha kamili ya washindi wa Tuzo hizo

  1. Best Male Artist: Diamond platinumz
  2. Best Female Artist: Nandy
  3. Best Hip Hop/Rap Artist: Elgrande Toto
  4. Hottest Group: Sauti Sol
  5. Best Collaboration: Beyonce ft Shatta Wale – King Already
  6. Best Music Video: Burnaboy – Anybody
  7. Entertainer of the Year: Eddy Kenzo
  8. Best Dancer/Group: Fire K Stars
  9. Best DJ: DJ Sinyorita
  10. Best Francophone Artist: Soul Bangs
  11. Best Palop Male Artist: Mr Bow
  12. Best Palop Female Artist: Yasmine
  13. Best New Artist: Laycon
  14. Song of the Year: Master KG – Jerusalema
  15. Best Upcoming/Local Artist: KG
  16. Best Male Artist – Central/ West Africa: Stonebwoy
  17. Best Male Artist – East/South/North Africa: Rayvanny
  18. Best Female Artist- Central/ West Africa: Yemi Alade
  19. Best Female Artist – East/South/North Africa: Zahara
  20. Best African Comedian: Eric Omondi
  21. Best Gospel Artist: Sinach
  22. Best Blogger/ Influencer: The Hot Jem
  23. Best Dance Hall Artist: Winky D
  24. Best Host TV/ Radio: Douglas Lwanga
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles